AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MKOANI MWANZA

Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani..
Upakuaji ukiendelea.
Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza. 



Meneja  Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na  Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  kwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo mapya Mwanza.










 

 




Post a Comment

0 Comments