Washindi
wa bahatinasibu ya Shinda Ki-Brazili na Mwanaspoti,Issa Rashid (wapili
kushoto) na Michael Msumba (wapili kulia) wakipokea zawazi zao kutoka
kwa Afisa Uhusiano wa Mult Choice ( Dstv ) Barbara Kambogi (kulia) na
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi,Edward Uisso.
Mwandishi Wetu, Dar
Kampuni
ya Mwananchi Communications Limited kupitia gazetilake la michezo la
Mwanaspoti kwa kushirikiana na DSTV wamekabidhi zawadi za washindi wa
kwanza wa ptomosheni ya Shinda Ki-Brazil iliyozinduliwa wiki iliyopita.
Washindi walizawadiwa ni
Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla ambao walizawadiwa
ving'amuzi na vifurushi vyake huku Jackson Fredrick wa Mwanza
akikabidhiwa jozi ya jezi yenye jezi 16.
Mbali ya kukabidhi zawadi
hizo, promisheni hiyo pia iliendesha droo na kupata washindi wapya.
Washindi wa vingamuzi vya DSTV pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa
mwezi mmoja (Compact Plus) waliopatikana ni Sharifu Migui (34) ambaye
ni Fundi Magari, John Kilalago (39) ambaye ni Mlinzi, Mahmud Salum (54)
ambaye ni Mtaalamu wa Takwimu wakati mshindi wa jozi moja ya jezi(ina
jezi 16) ni Bariki Massawe(38) ambaye kazi yake ni mfanyabiashara.
Migui ambaye ni mkazi wa
Mikumi Morogoro alisema, " Ninafuraha kushinda kwenye shindano hilo. Ni
kitu rahisi kupata kama mtu unashiriki kwani unakuwa umejijengea nafasi
ya kutosha endapo ninashiriki na mimi nimeshiriki mara nyingi ."
Massawe ambaye ni mkazi wa
Tabata Kinyerezi alisema," Nimefurahi kushinda jezi baada ya kushiriki
kwenye promosheni bomba ya Mwanaspoti. Jezi hizo nitatoa zawadi kwa timu
yangu ya maveterani inayoitwa Kinyerezi Veteran FC."
Afisa Masoko wa Kampuni ya
MCL, Edward Uisso, amesema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa
wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 24 za
DSTV zilizounganishwa na kifurushi cha Compact Plus kwa muda wa mwezi
mmoja, seti nne za jezi pamoja na fedha taslimu zinazotolewa kila siku
mpaka shindano litakapomalizika.
Promosheni hiyo ambayo
ilifunguliwa Juni 2 itafungwa Julai 13 siku ya mwisho ya fainali
hizo.Ili kuendelea kushiriki, wasomaji wa Mwanaspoti watatakiwa kutuma
namba zitakazopatikana kwenye ukurasa huu wa tatu wa gazeti la
Mwanaspoti kwenda namba 15551.
Kwa mujibu wa vigezo na
masharti ya promosheni hiyo, kila nakala ya gazeti la Mwanaspoti itakuwa
na namba mbili za ushiriki zenye tarakimu nane kila moja.
Mshiriki
ana hiari ya kutuma namba yoyote kati ya hizo kushinda aina moja ya
zawadi, au akipenda anaweza kutuma namba zote mbili ili kujishindia aina
zote mbili za zawadi.
Namba
moja imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye
droo ya zawadi za binafsi. Namba ya pili imetambulishwa kwa herufi T na
itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za timu.
0 Comments