Kikosi cha timu ya Biriadi Pool Table ya mkoani
Mwanza kinatarajia kuuwakilisha mkoa wa Mwanza katika michuao ya Pool ngazi ya Taifa
baada ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ngazi ya mkoa wa Mwanza baada ya kuibuka
na Pointi 13 kwa 11 dhidi ya Wanyama.
Reportage: Henry Kavirondo –
Mwanza:……………………………………………………….. ....
Katika mchezo huo kila ilikuwa imejidhatiti kutwaa
ubingwa huo, lakini jitihada za mchezo zilizoonyeshwa na kikosi cha Biriadi
Pool Table, ndizo zilizowawezesha kutengeneza historia ya kutwaa ubingwa huo msimu
huu dhidi ya Wanyama.
Kutokana na matokeo hayo timu hiyo pamoja Mwanadada
Rukia Issa, aliyefanikiwa kutwaa ubingwa kwa upande wa wanawake watauwakilisha
mkoa wa Mwanza katika michuano hiyo ngazi ya Taifa inayotarajiwa kufanyika
mkoani Kilimanjaro baadaye mwaka huu.
(1) BEKA
MBULA – Nahodha wa timu ya Biriad Pool Table.
(2) EMMANUEL
GOYA – Nahodha wa timu ya Wanyama.
Mratibu wa michuano hiyo Michael Machela amewaambia
waandishi wa habari kuwa tayari maandalizi yote ya michuano hiyo
yameshakamilika ambapo jumla ya timu kutoka mikoa 17 nchini zinatarajia
kushiriki katika michuano hiyo.
(3) MICHAEL
MACHELA – Mratibu wa michuano ya Pool Table kitaifa.
(4) BENARD
NAOMWISALIA - Mwakilishi wa Kampuni ya
bia Tanzania (TBL).
Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imejikita kudhamini
michuano ya Pool Table ngazi ya taifa ili
kuinua kiwango cha mchezo huo kimataifa lengo ikiwa ni kufungua milango
ya ajira kwa vijana.
0 Comments