Wachezaji wa Simba wakishangilia bao |
Golikipa wa JKT Oljoro akificha mpira baada ya kuudaka |
Amis Tambwe akikimbia na mpira huku Nurdin Mohamed akimkimbiza |
Uhuru Seleman wa Simba na Shaib Nayoba wa JKT Oljoro wakipambana |
Kikosi cha Simba |
JKT Oljoro |
Makocha wa Simba Loga na Matola wakisalimiana na kocha wa JKT Oljoro Hemed Morocco kabla ya mchezo kuanza |
Simba ya Dar es Salaam leo iliibuka na ushindi mnono
wa bao 4-0 dhidi ya Oljoro JKT katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku
mchezaji wake Amis Tambwe akifunga mabao matatu peke yake na kukabidhiwa mpira.
Washindi waliandika bao la kuongoza katika dakika ya
11 kupitia kwa Jonas Mkude baada ya kupigwa kona fupi na Ramadhani Singano na
kumkuta mfungaji aliuyeunganisha wavuni kwa shutu kali lililompita kipa wa
Oljoro Mohamed Ally.
Singano aliambaa na mpira upande wa kulia na kumpiga
chenga beki wa kushoto wa Oljoro Ally Omary na kupiga krosi iliyomkuta Amis
Tambwe akiwa pekee yake aliyeukwamisha mpira wavuni katika dakika ya 23.
Tambwe tena alicheka na nyavu katika dakika ya 29
baada ya kufunga kufuatia pasi kutoka kwa Amri Kiemba katikati ya uwanja na
kumpasia mfungaji aliyekimbia na mpira na kuwazidi mbio mabeki kabla ya
kufunga.
Katika kipindi cha kwanza Oljoro nusura wafunge baada
ya Shija Kina alikaribia kufunga lakini akiwa ndani ya eneo la hatari
alisukumwa na beki Donald Msoti lakini mwamuzi Nathani Lazaro wa Kilimanjaro kushindwa kuwapa penati.
Amiri Omary wa Oljoro alishindwa kuipatia timu yake
bao licha ya kuwa katika nafasi nzuri baada ya kubaki yeye na kipa Ivo Mapunda
kufuatia krosi safi ya Paul Malipesa, alishindwa kufunga na badala yake mpira
ulidakwa kirahisi na Mapunda.
Simba walianza kwa kasi kushambulia lango la wapinzani
na walifanikiwa kufunga bao katika dakika ya 56 na kujihakikishia `hat trick’
akimalizia krosi ya Haruna Chanongo kutoka upande wa kulia wa uwanja huo.
Simba waliutawala zaidi mchezo huo huku Oljoro
wakionekana wazi kukatishwa tama na kipigo hicho.
Mwamuzi alimkabidhi mpira Tambwe kutokana na kufunga
mabao hayo matatu katika mchezo mmoja, kitendo kilichoibua shangwe kwa
mashabiki. Tambwe katika zunguko wa kwanza alifunga mabao manne katika mchezo
dhidi ya Mgambo Shooting lakini mwamuzi wa mchezo huyo alimbania.
Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola alisema baada
ya mchezo huo kuwa, timu yake ilistahili kushinda lakini mchezo ulikuwa mgumu
kwani timu zilizomkiani zinataka kujanusua.
Alisema watajipanga vizuri kuhakikisha wanaendelea na
ushindi katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika kwenye
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Naye kocha wa Oljoro JKT Hemed Morocco alisema mchezo
ulikuwa mgumu kwani wachezaji wake walicheza vibaya katika kipindi cha kwanza
na kusababisjha kufungwamabao matatu, na aliwapongeza Simba kucheza vizuri.
Alisema kuwa Oljoro wampe muda zaidi wa kuandaa timu
kwani wachezaji wake wengi ni wageni, lakini atajitahidi kuhakikisha timu hiyo
haishuki daraja na inafanya vizuri msimu huu.
Timu zilikuwa:Simba:Ivo Mapunda, William Luciana,
Issa Rashid,Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo,Awadhi
Juma, Amri Kiemba/Said Ndemla, Amis Tambwe/Uhuru Selemani na ramadhani Singano.
Oljoro JKT:Mohamed Ali, Paul Malipesa, Ali
Omari, Aziz Yusuf, Nurdin Mohamed/Shaibu Nayopa, Sabri Makame/Swaleh Idd, Babu
Ally/Hamis Maulid, Jacob Masawe, Amir Omari, Shija Mkina na Majaliwa Mbaga.
0 Comments