VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI VYAUNGANA KUWAKUTANISHA MABONDIA JUMAMOSI


Vyama vya ngumi za kulipwa nchini  vimekubali  kuungana na wenzao TPBO kushiriki mkutano wa mapromota wa ngumi na mabondia wote wa Tanzania. Mkutano huo unaotarajiwa  kufanyika katika ukumbi wa vijana Kinondoni, siku ya jumamosi tarehe 1/2/2014 kuanzia  saa nne asubuhi. Mkutano huo ulioitishwa na TPBO chini ya udhamini wa KITWE GENERAL TRADERS ukiwa na lengo la kuweka mikakati ya sasa na ya baadae kwa ajili ya kuinua ngumi za hapa nchini,sanjali na kutambulikana kwa mapromota na mabondia wenyewe kwa kutengenezewa vyeti maalum na vitambulisho, vitakavyowafanya watambulike katika jamii ya wanamasumbwi wa hapa Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi yetu,hizo ni sehemu ya mada zitakazozungumzwa.
Ibrahim kamwe akizungumza na vyombo vya habari ,alisema ‘Mkutano huo ambao utawahusisha mapromota wote ,pamoja na viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa,makocha na mabondia wote wa ngumi za kulipwa, haijalishi wewe ni nani ili mradi ni mwalimu wa ngumi, mratibu wa ngumi au bondia ni vema ukafika katika mkutano huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika  katika historia ya ngumi za kulipwa kuwakutanisha kwa pamoja waratibu, viongozi na mabondia wa nchi nzima kwa pamoja, pia mkutano huo utaendana na mapromota kupewa vyeti  na kurekebisha usajili wa mabondia ambao usajili wao haujakaa sawa.

Post a Comment

0 Comments