Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014,
akikagua vitabu vya ziada. Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara ya
kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa kutokana
na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama
ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake ilikuta
vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi. |
0 Comments