Nilipopokea
mwaliko kutoka Mfuko wa Pensheni (PSPF) ukiniomba kuhudhuria kwenye
hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja na wadau wa tasnia ya sanaa na
michezo nchini, sikuelewa mara moja lengo la hafla hiyo lakini baada ya
kufika ukumbini na kupata ufafanuzi wa mabadiliko makubwa yaliyofanywa
na PSPF nikapata somo.
Kumbe PSPF sasa si kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.
Wadau wengi wa tasnia ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine wengii...
Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata
Steve Nyerere
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina
Martin anasema lengo kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa
uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu
yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe.
“Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani Main Scheme” Anasema Costantina
0 Comments