Wanakamati
wa kamati ya kumuaga mtangazaji mkongwe nchini, marehemu Julius Masiaga
Nyaisanga, Masou Masoud (kushoto) na Aboubakar Lyongo wakijadiliana
jambo kabla ya mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kuwasili katika
viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo, ambapo shughuli za
kuaga mwili zilifanyika kabla ya kuusafirisha mwili kwa mazishi katika
Kijiji cha Buhemba, Tarime Mkoani Mara. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya waombolezaji.
Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu.
Mtoto
wa marehemu Julius Nyaisanga, Samweli Nyaisanga (kushoto) akiwa na
baadhi ya wanandugu kabla ya kuagwa kwa mwili wa baba yake.
Mke
wa marehemu, Leah Nyaisanga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na wanafamilia ya Nyaisanga. Kutoka kulia ni mtoto wa marehemu,
Beatrice Nyaisanga na Samweli Nyaisanga.
Wanafamilia.
Mke wa marehemu, Leah Nyaisanga akiwa na watoto wake Samweli Nyaisanga na Beatrice Nyaisanga.
Msafara
wa magari ukiingia katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya
shughuli za kuaga mwili wa marehemu Julius Naisanga 'Acle J'
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Nyaisanga.
Waombolezaji.
Padri akimwagia maji ya baraka jeneza.
Regina Mwalekwa akisoma neno la Mungu.
Baadhi ya waombolezaji.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal akipeana mkono na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Makamu wa Rais akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akizunguka
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi akizungumza wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akitoa salamu za rambirambi.
Makamu wa Rais akitoa salamu za rambirambi.
0 Comments