Kutoka kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo Hillary Daudi a.k.a Zembwela akiwa na Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Udhamini Vodacom Calvin Twissa.
Mratibu wa ziara hiyo Hillary Daudi a.k.a Zembwela katika mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani leo(PICHA ZOTE NA BONGOWEEKENDBLOGSPORT.COM)
KUNDI la wasanii nyota
duniani la P-Square wanatarajiwa kufanya ziara
na onyesho kubwa jijini Dar es Salaam imefahamika.
Wasanii ambao ni mapacha
huku majina yao halisi ni Peter na Poul
Okoye watapiga shoo ya aina yake Novemba
23 mwezi ujao jijini Dar es Salaam katika eneo litakalotangazwa baadaye.
Akizungumza leo na
waandishi wa habari Mratibu wa ziara hiyo kutoka kituo cha luninga cha East
Africa (EATV), Hillary Daudi ‘Zembwela’alisema taratibu zote muhimu za ziara
hiyo zimekamilika.
Zembwela aliongeza kwa
kusema kuwa kuwa kundi hilo litakuja na wasanii
wao 13 ambao watapiga shoo ‘Live’, siku hiyo itakuwa ni ya kihistoria
katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
Ziara ya wasanii hawa
mapacha inaratibiwa na kwa ushirikiano wa EATV pamoja na kituo cha TV cha East
Africa na kudhaminiwa na Kampuni kubwa
ya simu nchini Vodacom.
“Lengo kubwa la kuwaleta wanamuziki hawa wanaoongoza kwa
umaarufu kila kona duniani kwanza ni kutoa burudani lakini
kingine kikubwa ni kuja kutoa somo kwa wanamuziki wetu hapa nchini namna ambavyo
muziki unaweza kufanyika katika hali tofauti na walivyozoea”.
Akizungumzia ziara hiyo
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Udhamini
Calvin Twissa wao kama wadhamini
wanajipanga kutoa tiketi za bure hivyo kazi kwa watumiaji wa Vodacom kwani
watatangaziwa namna ya kupata tiketi za bure kwenda kuwashuhudia vijana hao
machachari Psquare.
“Vodacom tunajivunia kuleta
kundi hili la wanamuziki wenye jina
kubwa duniani , mtakumbuka juzi tulisaini mkataba mnono na Naseeb Abdul
‘Diamond’ kupitia kibao chake cha Number One hivyo tunaahidi kufanya kazi na
wasanii wengine wengi wa hapa nyumbani” alimalizia Twissa.
0 Comments