Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jella Kheri Mambo, akiwa Ofisini kwake.
Ofisi ya Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini
Na Bryceson Mathias, Kondoa
KATIKA
hali inayoonesha ni kumliza Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM),
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kijiji cha Mlongila Kata ya
Jangalu, Jimbo la Kondoa Kusini, Kimeshinda kwa kishindo uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho.
Hatua
ya Chadema kuonesha kinakubalika hadi vijijini, kilishinda uchaguzi huo
uliofanyika Jumamosi, Agosti 24, ambapo Mgombea wa Chadema, Sariah
Bakari Lubuva Alishinda kwa kura 184 na kuwatupa mbali wagombea wenzake
baada Mwenyekiti aliyekuwepo kujiuzulu.
Akizumza
na Mwandishi wa habari hizi Katibu Mkuu wa Chadema mkoani Dodoma,
Stephen Masawe, alithibitisha mgombea wao Lubuva kushinda kwa kura
(184), dhidi ya kura za Chama cha Mapinduzi (CCM) waliopata (96) na
Chama cha wananchi (CUF) waliopata (9).
“Hizo
ni salamu na Mvua za rasharasha kwa Nkamia anayedai anapenda kuzungumza
na mwenye Mbwa badala ya Mbwa, lakini Chadema tunazungumza na Nguvu ya
Umma yenye Hati Milki ya Tanzania”.alisema Masawe.
Wakati
huo huo Kaimu Katibu wa Wilaya ya Dodoma Mjini (Chadema), Jella Kheri
Mambo, amekanusha Kauli ya Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma wanaomtuhumu
kuwa yeye na wenzake waliojiunga Chadema wako huko kwa Mkopo.
Alisema
Kauli ya viongozi wa CCM Mkoa ni ya Fisi aliyenyatia mkono wa mtu
akidhani utaanguka, lakini hadi safari inakwisha haukuangua naye
akaambulia Patupu asiupate.
“Nilikataa
zawadi ya uongo wa Ufisadi wa Makusanyo ya Mil.1,5/= badala ya Sh.
Mil.5/- zilizostahili kukusanywa kwa nyumba 500 za Kata ya Uhuru kila
nyumba 10,000/-. Viongozi hao wakafanya njama kuniondoa, hivyo siwezi
kurudi CCM“.alisema Mambo.
Aidha
badala yake Mambo amesema, hivi karibuni Chadema Dodoma Mjini kinaanza
kampeni maalum (M4C) ya Mlango kwa Mlango kuzungukia Kata 37 wilayani
humo,ili kuongeza Idadi ya wanachama wake, mbali ya wale inaowapata
kwenye Mikutano ya hadhara kila mara.
Nilikuwa
mmuumini wa Azimio la Arusha na sera za Chadema ni hizo ambazo mimi ni
muumini wake. Wananchi na Viongozi wapuuzeni CCM walioshindwa kuwatetea
wananchi badla yake wanawafanya watumwa wa kuwasomeshea, kuwalisha na
kuwavisha watoto wao”.alisema Mambo.
0 Comments