Mwandishi wetu
TIMU
ya soka na Netiboli za Waandishi wa Habari za michezo nchini, Taswa FC
na Taswa Queens zimemaliza maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kwa kishindo
baada ya kuwatambia wageni wao, timu ya Kiliflora ya Arusha.
Katika
mchezo wa soka, uliochezwa kwenye uwanja wa TCC Chan'ombe Taswa FC
iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 wakati katika mchezo wa netiboli
uliochezwa pia kwenye uwanja huo huo, Taswa Queens iliyokuwa inacheza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18 iliibuka na ushindi wa mabao 28-8.
Taswa FC ilianza mechi
hiyo kwa kasi na kufana mashambulizi ya mengi hata hivyo, washambuliaji
wake, Julius Kihampa na Shafii Dauda walikosa mabao mengi ya wazi.
Katika mechi hiyo, kipa
wa Taswa FC, Said Seif alikuwa ‘likizo’ kufuatia safu ya ulinzi chini ya
Muhidin Sufiani, Fred Mweta, Sweetbert Lukonge, Fred “Chuji” Mbembela
kuwa imara muda wote huku safu ya kiungo ilichezwa na Ali Mkongwe,
Wilbert Molandi, Majuto Omary na Evarist Hagila kutotoa mwanya kwa
Kiliflora kupenya na kupeleka mashambulizi.
Baada ya kosa kosa hizo,
Taswa FC iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 24 kufuatia
gonga safi za Majuto “Ronaldo De Lima” Omary na Ali Mkongwe kabla ya
mpira kumfikia Hagila na kuuweka kimiani.
Bao hilo lilionekana
kuwachanganya Kiliflora na kujikuta wakipachikwa bao la pili kupitia kwa
Dauda baada ya pasi nzuri ya Wilbert Molandi aliyecheza vyema na Sweetbert Lukonge na kufanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0 mpaka mapumziko.
Taswa Fc ilifunga bao la
tatu kupitia kwa Hagila baada ya pasi kupata pasi safi ya Fred Mbembela
‘Chuji’ na baadaye Dauda kufunga la bao la nne kufuatia ngazi nzuri ya
Majuto.
Katika netiboli,
ikiongozwa na Imani Makongoro aliyecheza nafasi ya (GS), Taswa Queens
iliifunika kabisa Kiliflora Queens baada ya kuongoza kwa 16-3 hadi
Mapumziko.
Wachezaji wengine wa Taswa Queens waliocheza mechi hiyo mbali ya Imani ni Oliver (mwananchi), Sada Ayoub, Johari
William, Elizabeth Mbassa, Shaarifa Mustapha wote wakitokea Business
Times. Timu hiyo ilikuwa chini ya makocha, Amina Mussa (BTL) na Zainab
Ramadhan (TBC).
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akikagua timu ya Netiboli ya Kiliflora ya Arusha, kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, akikagua timu ya Netiboli ya TASWA Queens, kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana.
Picha ya juu ni TASWA Fc katika picha ya pamoja na ya chini ya
Kiliflora ya Arusha, kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana. Picha Zote na Nasma Mafoto
www.sufianimafoto.com
0 Comments