Rais wa TALISS Swimming Club
Bi. Najat Saleh Ahmed (mwenye miwani nyeusi) akizungumza na washiriki
pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea
yaliyoshirikisha Club mbalimbali na kwa rika tofauti yaliyodhaminiwa na
Kampuni ya CFAO Motors wauzaji wa magari ya kisasa hapa nchini
yaliyofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya
Tanganyika (IST).
Amesema Mashindano hayo
hufanyika kila mwaka na kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi
wa kuogelea unaofikia kiwango cha kushiriki mashindano.
Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba
wadau zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali
ijitokeze na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza
kuogelea ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.
Pichani juu na chini washiriki wa club mbalimbali za kuogelea wakipita mbele wazazi na makocha kwa ajili ya utambulisho.
Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
Pichani juu na chini ni
washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya
kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya
CFAO Motors ya jijini Dar.
Picha juu na chini Sehemu ya
watazamaji wakishuhudia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
0 Comments