Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish
Airlines Dkt.Temel Kotl akishuka kwenye ndege ya Turkish Airlines aina ya
B737-900 wakati wa hafla uzinduzi wa safari ya ndege hiyo ya
Instabul-Kilimanjaro iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mngodo (wanne
kushoto) akikata utepe kuzindua safari ya Shrika la Ndege la Turkish Airline
kwenye Uwanja wa KIA jana. Watatu kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines
Dkt.Temel Kotl.
Baadhi ya abiria wakishuka akishuka kwenye ndege ya
Turkish Airlines aina ya B737-900 wakati wa hafla uzinduzi wa safari ya ndege
hiyo ya Instabul-Kilimanjaro iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la
Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya
KADCO Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines
Dkt.Temel Kotl wakati wa hafla uzinduzi wa safari ya ndege ya Turkish Airlines
ya Instabul-Kilimanjaro katika hafla siliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa
KIA.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la
Ndege la Turkish Airlines limeanza rasmi kutumia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa safari zake za
Instabul-Kilimanjaro – Mombasa kufuatia jitihada za kuboreshwa na
kutangaza uwanja huo zinazofanywa na kampuni inayoendesha uwanja huo ya
Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO).
Shirika hilo
ambalo litafanya safari mara tano kwa wiki liaungana na kampuni za ndege
nyingine za Qatar Airways, Qatar ,KLM,Edelweiss Air, Condo Air na
Ethiopian Airlines ambayo tayari yamezindua safari zake kupitia uwanja
huo.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Safari ya Shrika la Ndege la Turkish
Airlines kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA jana, Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO
Balozi Hassan Kibelloh alisema mvuto wa uwanja huo umetokana na
jitihada za makusudi zilizofanya na kampuni yake ilikuufanya uwanja huo
kuwa na muonekano wa kimataifa.
“Tunashukuru
kwa ujio wa ndege hii ya kimataifa ya Turkish Airlines. Ujio ha ndege
hii unatupachangamoto ya kuendelea kuboresha huduma zetu ilituendelee
kuvutia ndege nyingine za kimataifa,” alisema.
“Hi ni ishara
kuwa Shirika la Turkish Airlines lina imani na uwanja wetu na itatoa
fursa nzuri kiushindani. Kutua kwa ndege hii kutaiunganisha Tanzania na
nchi nyingine jirani katika masoko yapatikanayo Marekani, Canada na nchi
za Ulaya kupitia mtandao mkubwa wa Shirika la Ndege la Turkish.
Nae Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Turkish Airlines Dkt.Temel Kotl
wakati wa hafla hiyo alisema kuwa kampuni yake ina imani kubwa na bara
la Afrika nakuongeza kuwa wanatarajia kufungua safari nyingine saba
kwenye bara la Afrika siku zijazo.
“Tuna imani
kubwa na soko liliopo kwenye bara via Afrika na lego letu kubwa kwa sasa
ni kuunganisha bara la Afrika na nchi nyingine zaidi duniani. Kwa
kuliangalia hilo, tunategemea kuaanzisha safari nyingine saba kwenye
Bara la Afrika,” alisema.
Naye Balozi wa
Uturuki ncini Ali Davutoglu wakati wa shuguli hiyo alisema nchi yake
imesaidia ukuaji wa sekta mbali mbali Barani Afrika zikiwemo elimu,
biashara na kilimo.
“Ushirikiano
wetu kibiashara na Bara la Afrika unakua kwa kasi sana. Mapato kupitia
biashara kati ya Tanzania yamekuwa kutoka dola milioni 18 mwaka 2004
mpaka dola milioni 198 mwishonmi wa mwaka 2011,” alisema.




0 Comments