MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA APIGWA RISASI NA POLISI




 Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Shaban Matutu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa risasi kifuani aliyopigwa na Polisi nyumbani kwake Tegeta.
 Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Shaaban Matutu akionesha jeraha lililotokana na kupigwa risasi na Polisi katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo - baada ya polisi kuvamia nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumtafuta mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka. Matutu kwa sasa amelazwa Hospitali ya Muhimbili katika Kitengo cha Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Shabaan Matutu akionesha sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upange wa kushoto wa kifua chake.
 Daktari aliyekuwa zamu katika Hospitali ya Mwananyamala akiangali picha ya X-Ray ya Matutu mara baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo na kufanyiwa kipimo hicho, kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Wafanyakazi wa Free Media Limited ambao ni wachapishaji wa  Khadija Kalili kushoto na Maria Kayala (kulia) ambao walifika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kupata taarifa za tukio hilo. 

Post a Comment

0 Comments