KESI
ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael
(Lulu), dhidi ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, inaendelea
kupigwa kalenda kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika. Kesi hiyo
iliahirishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya
Hakimu Mkazi, Augustino Mbando. “Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi
hii haujakamilika, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alidai Wakili
wa Serikali, Kenneth Sekwao. Hakimu Mbando alikubali kuahirisha kesi
hiyo hadi Desemba 17 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa. shitakiwa
anatetewa na mawakili, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatara na Fulgence
Masawe. Lulu yuko rumande kwa miezi nane sasa kutokana na makosa ya
mauaji na kukosa dhamana, anadaiwa kwamba Aprili 7 mwaka huu maeneo ya
Vatican, Sinza, alimuua Steven Kanumba. Kuchelewa kukamilika kwa
upelelezi kumeanza kuzua mjadala kwa watu mbalimbali wanaofika
kusikiliza kesi hiyo, wakidai kwamba hawajui matukio gani nchini ambayo
upelelezi wake unaweza kufanywa kwa haraka. “Nashindwa kuelewa, kila
siku upelelezi bado, kuna upelelezi gani katika kesi hii wa kumaliza
mwaka mzima, kila kesi ina mazingira yake ya kuchelewesha upelelezi
lakini hii…” alihoji msikilizaji huku akitoka katika chumba cha
mahakama.
MBUNGE, DC NA DAWASA WASAKA SULUHU YA MAJI KIBAMBA
-
Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC) pamoja na
watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam
(DAWASA) wamekutan...
CHUMBI A MKOA WA PWANI WAPANDA MITI
-
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, ameongoza wakazi wa Chumbi
A, Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, katika zoezi la upandaji miti ikiwa ni
sehemu...
TANZANIA: THE ULTIMATE ENSEMBLE
-
From the raw adrenaline of the Mara River to the spice-scented tranquility
of the Indian Ocean—this is 6 days of pure "Hospitality Highness."
Why c...
Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera
-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua
chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani
Kagera k...
0 Comments