Msanii wa filamu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Filamu cha Tanzania Film Training Centre (TFTC) Emmanuel Myamba maarufu kama Pastor Myamba akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kushoto kwake ni Katibu wa Shirikisho la Filamu nchini Wilson Makubi
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo akisisitiza jambo wakati akihitimisha programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii.Kulia kwake ni Kaimu Mratibu wa Jukwaa hilo Agnes Kimwaga
Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Mzee Kassim Mapili naye alitoa nasaha zake kuhusu tasnia ya filamu
NaMwandishi WetuWadau wa Sanaawamehoji uhalali wa wasanii wa filamu kutumia kiingereza kwenye majina yafilamu zao huku wakishangazwa na kazi hizo kubeba maudhui ya kizungu zaidi.
Wakizungumza wiki hiikwa nyakati tofauti kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa, wadau hao walishangazwakitendo cha filamu hizo kutumia majina ya kizungu wakati hapa kwetu kuna filamunyingi kutoka nje zinazotumia lugha za kihindi, kichina, kifaransa na zinafanya vizuri.
“Hoja kwamba,wanatumia majina ya kiingereza ili kuteka soko la kimataifa ni ya kitoto, mbonahapa kwetu kuna filamu nyingi za kihindi na kichina zinanunuliwa kwa wingi? Hapakuna udhaifu katika kutengeneza filamu zenye ubora tujikite huko”alisema MzeeNkwama Bhallanga.
Kwa mujibu wa wadauwengi waliozungumza, filamu ni taaluma inayozungumza kwa kutumia picha navitendo zaidi hivyo haihitaji mtazamaji kufahamu lugha iliyotumiwa ili afahamumaudhui na ujumbe unaowasilishwa na kazi husika ya filamu.
“Maneno kwenye filamusi muhimu sana, kinachozungumza ni matendo na picha zaidi, ndiyo maana kunawatu wanaangalia picha za Kikorea na wanaburudika na kuelewa kinachoendelea”alisema Godfrey Lebejo ambaye ni Murugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo nahabari, BASATA.
Aliongeza kuwa,kinachoitesa tasnia ya filamu kwa sasa ni kukosekana kwa weledi na uhalisia watamaduni zetu kunakosababishwa na wimbi kubwa la watu kujiingiza kwenye filamu ilikufanikisha mambo yao yaliyo nje ya maadili na utamaduni wetu.
“Inawezekana vipiutengeneze filamu ambayo baba, mama na watoto hawawezi kukaa pamoja kuitazama?Tufike mahali tuseme mambo haya ya kipuuzi basi kwenye filamu zetu” alionyaLebejo.
Awali akiwasilishamada kuhusu Filamu, wasanii na haja ya kujiendeleza kielimu, Msanii wafilamu Emmanuel Myamba maarufu kam Pastor Myamba alisema kuwa, tasnia ya filamuinakosa weledi hivyo kuhitaji mabadiliko.
“Ni wazi ukiangalia filamuzetu zinakosa weledi katika uandishi wa miswada, uongozaji, uhariri na hatauumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe” alisema Myambaambaye kwa sasa amefungua kituo cha mafunzo ya filamu kiitwacho Tanzania FilmTraining Centre (TFTC) kilichoko Ubungo.
0 Comments