Mlinzi wa Timu ya Soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,YonaKirumbi akiwa amemnyang'anya mpira,Fuad Rashid wa Timu ya Baraza laWawakilishi Zanzibar,katika pambano lililochezwan kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam juzi jioni kugombea kombe la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Timu ya Bunge ilishinda kwa bao4-1..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Mwinyi Haji Makame akikabidhi kombe la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwa Amos Makalla Nahodha wa Timu ya Soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Timu hiyo iliilaza timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar,bao 4-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam jana. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia nya Serengeti(SBL), Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa Masoko, Ephraim Mafuru na meneja wa vinywaji vikali,Emilian Rwejuna.
(Picha Zote na Mohamed Mambo).
Adam Malima wa Timu ya Soka ya Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikabwa na Fuad Rashid wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar,huku Yona Kirumbi (kulia)akijiandaa kusaidia.Pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanjawa Taifa, Jijini Dar es Salaam juzi jioni kugombea kombe la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
0 Comments