BENKI YA AZANIA YADHAMINI TOTO PARTY YA FUNGA MWAKA 2011

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo Cha kulelea Watoto yatima Tupendane kilichopo Manzese Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya GLITZ Entertainment  Limited Ssebo na Ofisa wa Benki ya Azania Othman Jibrea ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Party hiyo ya watoto iliyopangwa kufanyika Jumamosi ijayo Desemba 17 2011 Cine Club Mikocheni.Ssebo alisema lengo la Party hiyo ya watoto ni  kuwakutanisha watoto  kutoka katika pande mbalimbali  za Jiji la Dar es Salaam.
"Katika Toto Party hii tutajumuika na watoto yatima kutoka katika kituo cha Tupendane kilichopo Manzense pia watoto 100 watakaowahi kufika watapata zawadi ya kufunguliwa Akaunti  bure huku jambo la muhimu ni kwamba kila mzazi atembee na vielelezo muhimu vya mtoto kama vile cheti cha kuzaliwa.Toto Party hiyo imepangwa kuanza saa3 asubuhi hadi 12 jioni.
Michezo itakayopatikana katika ufukwe huo ni pamoja na mashindano ya kuimba, kucheza,  kujibu maswali, hide& seek, face painting, jumping castle na minghineyo mingi yenye mvuto kwa watoto.Ulinzi wa kutosha upo.Kiingilio kwa watoto ni sh.3,000 na wakubwa sh. 6,000.Wadhamini wengine Totoparty ni gazeti la Jambo Leo, Channel Ten, Magic FM, na Clouds FM. 


Post a Comment

0 Comments