BAADA YA KUFANYA MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU UK SASA TWANGA WARUDI NYUMBANI

Kutoka shoto ni mpiga drums Martin Kibosho, Chiriku wa Twnaga Charlz Gabriel 'Charls Baba' na mnenguaji Asha Said 'Sharapova' wakitoka nje ya mlango katika Uwanja wa Ndege wa Mwal.JK. Nyerere leo asubuhi.

 Mpapasa Kinanda Victor Mkambi  'Professional Keyboad' kimwaga tabasamu 'Home Sweet Home' au siyo.
 BENDI ya Muziki wa dansi The African Stars “Twanga Pepeta International ” wamerudi nchini jana alfajiri baada ya kufanya maonesho yake yaliyofana ya nchini Uingereza kwa ajili ya ziara ya kimuziki ya miaka 50 ya Uhuru.Twanga waliwasili nchini leo asubuhi kwa Shirika la Ndege la Uingereza Britisha Airways.

Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu ‘Mama B’ alisema mara baada ya kuwasili  kwamba maonyesho yao ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru yalifana sana na kwamba wametoa shukrani zao za dhati kwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe na watanzania wote kwa ujumla.

“Tulipokuwa nchini Uingereza Twanga Pepeta ilifanya maonesho matatu makubwa katika miji tofauti ya London. Milton Keynes na Birmingham” alisema Mbutu..
Alisema onesho la kwanza ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya ufunguzi wa sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika nchini Uingereza ambalo lilihudhuriwa Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Peter Kallaghe, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na Kaimu Balozi Kilumanga.
Aidha katika ziara hiyo Twanga Pepeta ni kufuatia mwaliko wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Jamii ya watanzania waishio nchini Uingereza chini ya Uratibu wa Urban Pulse na Miss Jestina Blog wakishirikiana na ASET.

Mbutu aliongeza kwa kusema kuwa wakiwa huko wamezindua albamu yao ya 11 inayokwenda kwa jina la Dunia Daraja ikiwa katika Video na Audio.
Hii ni mara ya pili kwa Bendi ya Twanga Pepeta kuzuru Uingereza mara ya kwanza ilikuwa mnamo mwaka 2007. licha ya kuzuru Uingereza Twanga Pepeta ilishawahi kuzurru Nchi mabalimbali za Bara la Ulaya kama Uholanzi, Norway na Sweden kwa lengo ya ziara ya kimuziki.

Mara baada ya kurejea chini Twanga Pepeta inataraji kuungana na wenzao waliobaki kufanya maonyesho yao ya kila wiki kwa kuanzia Jumatano watakuwa Club Billicanas, Alhamis watakuwa Equator Grill Mtoni, Ijumaa watasherehekea miaka 50 ya Uhuru katika ukumbi wa Da West Park uliopo maeneo ya Tabata. Jumamosi watakuwa Mango Garden Kinondoni na Jumapili mchana wataanzia kutoa burudani katika Bonanza Leaders Club Kinondoni na baadae watakuwa Msasani Beach Club.

Twanga Pepeta iliondoka na wasanii 12 ambao ni Kiongozi Mkuu Luizer Mbutu, Kiongozi Msaidizi Saleh Kupaza, Charles Baba, Venance na Khamis Amigolas. Wengine ni Miraji shakashia, James Kibosho, Victor Nkambi na Jumanne Jojoo. Wengineo ni Asha Said “Sharapova”, Maria Soloma na Betty Johnson “Baby Tall”
 Katikati ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya ASET inayomiliki bendi hiyo Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.
 Salehe  Kupaza 'Mwana Tanga' akionyesha machejo kidogoo  pia amesema akiwa nchini Uingereza ametunga wimbo mmoja mkali ambapo anapingana na dhana isemayo Uzuri wa Mwanamke ni jinsi alivyo na siyo tabia huku akiachia mistari yake kidogo kwa kusema kuwa , Uzuri wa mwanamke ni jinsi alivyo ndiyo kwani ni vigumu kuijua tabia yake kwa kumwangalia.Wimbo huo anausuka na utakuwa tayari kabla ya mwaka haujaisha
.Bongoweekend kama kawa nikaenda kumpokea shosti 'Mashauzi Original' Luiza Mbutu  'Mama B' .

Post a Comment

0 Comments