Mbwa wa polisi akiwa uwanjani peke yake baada ya kuwafukuza wachezaji.
Ndani ya Uwanja wa CCM kirumba mwanza lilitokea tukio la aina yake baada ya Mbwa wa Polisi kuingia uwanjani na kuanza kukimbiza wachezaji wakati wa mechi ya Simba na Toto Africa
Kitendo kama hiki cha kizembe ni nani alaumiwe! na TFF imesemaje ili kisitokee tena?
Kwa uelewa wangu Mbwa wa polisi akipelekwa kwenye shughuli za Soka anatumika tu kwa ajili ya kutishia wale ambao wanataka kukiuka taratibu, lakini sio kwa kumuachia kama hivi. Kama hii mechi ingekuwa ni ya Kimataifa TFF wategemee nini kutoka FIFA! au Fideration ambayo itakua imeandaa mashindano hayo!
"TUWE NA UTARATIBU WA KUWAPA SEMINA HAWA WOTE WANAOHUSIKA NA SHUGHULI HIZI"
KAPINGAZ Blog imesikitishwa na tukio hili.
0 Comments