Kushoto Mkurugenzi wa Kampuni ya PAPA ZI Zacharia Pope akiwa na Makurugenzi wa Kampujni ya Lino International Agenncy ambayo inaratibu shindano la Miss Tanzania Hashim Lundenga.
KAMPUNI ya Papa Zi Entertainment inayojishughulisha na kazi za burudani nchini hasa katika Sanaa ya Filamu wamejitosa kwa kutoa udhamini katika sindano la Miss Tanzania.“Kampuni yetu ni kubwa na yenye mtaji mkubwa ikiwa na lengo la kumkomboa msanii wa Tanzania ili apate kipato kizuri” alisema Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Zacharia Pope.Leo hii tupo hapa kama wadhamini washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2011. Lengo letu ni kujitangaza na kutoa fursa kwa Wasanii kujiunga na kujivunia Kampuni yetu hii ambayo kwa kiasi ni mkombozi kwa wasanii wa sanaa ya urembo na filamu kama nilivyoainisha hapo juu. Kama Wadhamini wenza Papa Zi Entertainment tunalengo la kutoa ajira kwa warembo watatu ambao moja kwa moja na kufanya kazi na Kampuni yetu. Tunatarajia kutoa zawadi ya pesa taslimu ya dola 1000 [USD] kwa mrembo atakaeshinda taji la Balozi wa Kampuni ya Papa Zi Entertainment ambalo utaratibu wa kumpata Balozi huyo tutashirikiana na Waandaaji wa shindano hili la Taifa, Kamati ya Miss Tanzania. Ni matarajio yetu kwamba Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania bw. Hashim Lundenga pamoja naKamati yako mtatupa ushirikiano wa kutosha. Mwisho tunaahidi kushirikiana na Waandaaji pamoja na Wadhamini wenza wengine katika kufanikisha shughuli mbalimbali kuelekea Fainali za Taifa za Vodacom Miss Tanzania 2011. Wadhamini wengine wa shindano hilo ni Vodacom, Redds, Giraffe Hotel, Star TV, New Habari 2006 Limited.
WAZIRI DKT. CHANA ACHANGIA MILIONI 6 KUWEZESHA SHUGHULI ZA UWT LUDEWA
-
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe Mhe.
Balozi, Dkt. Pindi Chana, Januari 11 2025 ameshiriki katika Baraza la Umoja
wa W...
1 hour ago
0 Comments