WASHIRIKI wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 wameiva na wako tayari kwa ajili ya fainali za Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 zinazotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Julai 7,2011.Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Yummie uliopo ndani ya ukumbi wa Vijana Hostel Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya ASET, Asha Baraka alisema vimwana kumi ambao wako tayari katika kuwania duka ambalo ndiyo zawadi kwa mwaka huu.
Tumebadilisha mtindo wa zawadi hivyo mashindi mwaka huu badaya la kumpa gari ambalo akigonga ndiyo inakuwa mwisho wa safari hivyo uopngozi wa ASET kwa kushirikiana na Manywele Entertainment tumeamua kutoa zawadi ya Duka lenye thamani ya sh. Mil.5 sambamba na kumlipia kodi ya mwaka mmoja.
“Jina la duka bado halijafahamika lakini katika kipindi chote mshindi atakuwa chini ya uangalizi wa ASET na Manywele katika kumpa miongozo ya biasha kwa ujuma” alisema Asha.
Mshindi wa pili atapata kitita cha sh.500,000, mshindi wa tatu atapata sh.300,000.
Wemgine watakaobaki yaani kuanzia wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh.100,000.
Mratibu wa shindano hilo Maimatha Jesse alisema kuwa burudani zitakazonogesha hindano hilo ni pamoja na kundi la Ze Comedy, Mwanamuziki AT na bendi ya Twanga Pepeta International.
Maimatha anawataja washiriki watakaochuana katika fainali hizo ni wale walioingia katika kumi bora ambao ni pamoja na Leila Mshana, Mary Hamis, Mariam Mwakyoma, Amina Juma, Hawa Miraji, Amanda Cyprian, Rehema Said, Johari Juma, Edina Amani na Salha George.
Washiriki hao watachuana katika miondoko ya Chunga Ng’ombe, Mugongomugongo na kila mshiriki atacheza katika miondoko ya Freestyle muda atakaopewa , pia katika kuongeza madoido washiriki hao wameongezewa Mwalimu wa kuwafundisha Bakari Kasongo ‘Mandela Surambaya’ kucheza ili waweze kufanya vizuri katika fainali za Shindano hilo ambaye ataongeza nguvu kwa kushirikiana na Kassim Mohammed au "Super K".
MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI GHANA KUSHIRIKI UAPISHO WA RAIS MTEULE MAHAMA
-
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Anwani ya simu:“MAKAMU”, Mji wa Serikali, Simu Na.: +(255)026 2329006 Eneo
la Mtumba, Nukushi....
5 hours ago
0 Comments