UZINDUZI wa shindano la urembo kumsaka Miss Mwanza 2011, unatarajiwa kufanyika Juni Mosi, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Crest iliyopo katika jengo la PPF, katikati ya Jiji la Mwanza. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, waandaaji wa shindano hilo, John Dotto, uzinduzi huo utaambatana na utambulisho wa warembo watakaochuana katika kinyang’anyiro hicho. Alisema kuwa tayari warembo wameshaanza kujiandikisha kuwania Umalkia wa Mwanza na kwamba wanaojiona kuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo, wanakaribishwa ambapo fomu zinapatikana katika ofisi za hoteli hiyo. “Bado tunakaribisha warembo wenye sifa kujiandikisha kwa sasa kwani baada ya uzinduzi, hatutapokea mrembo yeyote yule, hata awe na sifa kiasi gani,” alisema. Alisema kuwa shindano lao linatarajiwa kuwa la kiwango cha juu, kuanzia maandalizi yake, warembo na shoo ya kilele cha kinyang’anyiro hicho. Dotto alisema kwamba lengo lao mwaka huu ni kumtoa Miss Tanzania kama ilivyokuwa miaka ya 2008 na 2009, wakiamini hilo linawezekana kutokana na jinsi walivyojipanga. Warembo waliotokea Mwanza na kutwaa taji la Miss Tanzania na miaka yao katika mabano, ni Nasreen Karim (2008) na Miriam Gerald (2009) ambao walikatisha kutamba kwa Jiji laDar es Salaamkatika mashindano hayo kutokana na kutwaa taji la Miss Tanzania mara nyingi zaidi. Dotto alisema: “Wadhamini wanaendelea kujitokeza na kwamba hadi sasa tunao PSI, Vodacom Tanzania na Redd’s, wengine wanakaribishwa kujitokeza kudhamini shindano hilo lenye historia ya kutoa Mrembo wa Taifa kwa miaka mwili mfululizo, 2008 na 2009.”
NBAA YAPAA KIMATAIFA
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeshiriki
mkutano wa Baraza la Shirikisho la Wahasibu Duniani (IFAC Council 2024)
unaof...
NBAA YAPAA KIMATAIFA
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeshiriki
mkutano wa Baraza la Shirikisho la Wahasibu Duniani (IFAC Council 2024)
unaofan...
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MAZISHI YA MZEE JOHN TUTUBA
-
*Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa marehemu John Tutuba ambaye ni
Baba...
DUKA JIPYA LA AIRTEL LAZINDULIWA JIJINI DAR
-
Mtendaji Mkuu wa TRC, Masanja Kadongosa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
duka la Airtel katika kituo cha Treni ya Kisasa kilichopo jijini Dar es
Salaam...
Cara Terbaik Untuk Menang Judi Sicbo Online
-
Bergabung dalam permainan judi sicbo online yang dapat dimainkan melalui
smartphone, maka tentu saja para pemain bisa melakukan sejumlah taruhan
dengan nya...
Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera
-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua
chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani
Kagera k...
0 Comments