Social Icons

Friday, April 29, 2011

SHINDANO LA MISS TANZANIA LAZINDULIWA RASMI KILIMANJARO KEMPINSKI DAR ES SALAAM USIKU HUU

Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala akiwa katika picha ya paoja na warembo waliowahi kuvaa Crown ya Miss Tanzania anaye fuata baada ni Angela Damas, Nasreen Karim, Jacqueline Ntuyabaliwe, Hoyce Temu, Saida Kessy na Richa Adhia.


WAREMBO TANZANIA 2011 KUKA KATIKA JUMBA , MASHABIKI KUWAPIGIA KURA
Kampuni ya simu ya kiganjani ya Vodacom juzi usiku wamezindua nembo mpya sanjari na kuzindua shindano la urembo la Miss Tanzania 2011.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja udhamini wa Kampuni hiyo George Rwehumbiza alisema kuwa Kampuni yake ndiyo mdhamini mkuu wa shindano hilo.Rwehumbiza alisema kuwa Kampuni yake inadhamini shindano hilo kwa lengo la kuikuza tasnia ya urembo sanjari na kukuza vipaji vya warembo hapa nchini.“Leo ni siku muhimu sana katika fani ya urembo hapa nchini kwani ni siku ambayo Kampuni yetu inazindua rasmi shindano la mwaka huu pamoja na nembo (Logo) yetu kwa mwaka huu” alisema.Aliongeza kwa kusema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni Urembo halisi (New Glamour and Elegance).
Aliongeza kwa kusema Kampuni yake ina imani kwamba kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma shindano la mwaka huu pia litakuwa na ushindani wa hali ya juu na kwamba atapatikana mrembo bora atakaye iwakilisha nchi katika shindano la dunia.“Natoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano vijana wao wenye nia ya kushiriki katika shindano hili na hivyo kuonyesha vipaji vyao.Pia nachukua fursa hii kuwaomba wasichana kokote walipo hapa nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shindano hili ili kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika kuitumikia jamii yetu” alisema.
Alisema shindano hilo ni muhimu sana kwani hulipatia taifa mwakilishi katika shindano la dunia.“Kama ada shindano hili litaanzia katika ngazi za vitongoji , wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa ambako ndiko kutakuwa na kambi maalum ndani ya nyumba ya Vodacom”alisema.
Alimalizia kwa kusema kuwa shindano la mwaka huu, litakuwa na mvuto wa aina yake kwani warembo 30 watakaoingia fainali hawataweka kambi hoteli kama ilivyozoeleza, bali watakaa kwenye nyumba maalum ijulikanayo kama nyumba ya Vodacom.
“Wakiwa humo wataonyesha vipaji mbalimbali na kuwapa fursa watanzania kuwapigia kura” alisema.Kwa wale wa mikoani watapata fursa ya kujifunza ujasiriamali chini ya wataalam wa Shirika la kuendeleza Viwanda vidogovidogo hapa nchini (SIDO) , baada ya kujifunza ujasiriamali huo wataweza kutumia ujuzi na vipaji vyao katika kuendeleza maisha yao wakiwa uraiani. Wadau hawa wakifuatilia uzinduzi wa mashindano haya ya urembo ambayo yamezinduliwa rasmi.
Mratibu wa Miss Tabata Fred Ogot akiwa na Miss Tabata 2010 Consolata Lukosi.


Mbunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi nchini Ally Rhemtullah. Muandaaji wa Kituo cha Kurasini Miss Kurasini Bibie Zuwena naye alikuwepo.



Somoe Ng'itu kulia na Khadija Kalili.

Mhariri wa Habari za Michezo na Burudani Suleiman Mbuguni na mimi. Mama wa Bongoweekendblog nikijiegesha nje mara baada ya hafla hiyo.





Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency pia Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Dar es Salaam.

Kampuni ya Viodacom usiku huu imezindua rasmi shindano lake la urembo la Miss Tanzania kwa kipindi cha maka 2011.Hapa Meneja udhamini wa Kampuni hiyo George Rwehumbiza amesema kuwa wao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo.Waliosimama nyuma yake ni baadhi ya warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.

Meneja Udhamini wa Kampuni hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano vijana wao wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo na hivyo kuonyesha vipaji vyao ."Pia nachukua fursa hii kuwaomba wasichana kokote walipo hapa nchini wajitokeze kwa wingi kushiriki katika shindano hili na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika kuitumikia jamii yetu".

Hawa ni baadhi ya warembo Miss Tanzania ambao walikuwepo katika uzinduzi wa rasmi wa shindano na nembo mpya ya mdhamini wao Kampuni ya simu ya Vodacom waling'ara kwa miaka tofauti na kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya dunia .Kutoka kushoto ni Angela Damas Miss Tanzania (2001),Nasreen Karim (Miss Tanzania 2009),Jacqueline Ntuyabaliwe (Miss Tanzania 2000),Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997).

Hapa tukishangweka SHOSTITO Miss Tanzania 1999 pia alikuwa Miss Ilala kwa mwka huo Hoyce Temu asiyechuja , Dina, Khadija nyuma ya Hoyce na menye kivazi cha buluu ni Somoe.

Mbunifu wa mitindo ya mavazi nchini Ally Rhemtullah katika uzinduzi huo .

Kutoka kushoto ni Dina, Mambo na Suleiman wote kutoka gazeti la Majira na Khadija.

No comments:

 
 
Blogger Templates