MAPATO SIMBA vs MAJIMAJI

Mechi namba 132 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Majimaji iliyochezwaAprili 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 19,799,000.


Mapato hayo ni kutokana na watazamaji 4,611 waliolipa kutazama mechi hiyo.Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 15,000 kwa VIP A, sh. 10,000 VIP B nash. 7,000 VIP C. Sehemu nyingine zilizobaki kiingilio kilikuwa sh. 3,000.


Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh.3,020,186.44 fedha iliyobaki kwa mgawanyo kwa pande zote husika ni sh.16,778,813.56.


Gharama za awali za mchezo kabla ya mgawanyo ni sh. 5,366,605.36. Gharama hizozinahusisha asilimia 10 ya uwanja, mjenzi wa uwanja kampuni ya BeijingConstruction, uchapaji tiketi, nauli za ndani na malazi kwa kamishna na waamuzi,jichangie kwa kila klabu na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA), umeme, ulinzi na usafi. Mgawanyo baada ya gharama hizo kila timu ilipata sh. 1,253,817.91, Shirikisho laMpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.


417,939.30, gharama za mchezo sh. 417,939.30,Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 37,994.48, DRFA sh. 189,972.41 na Mfuko waMaendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 227,966.89.


Boniface Wambura


Ofisa Habari TFF

Post a Comment

0 Comments