Social Icons

Saturday, April 16, 2011

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI 'WATER FOR LIFE' ULIODHAMINIWA NA KAMPUNI YA EABL

Hapa ni mara baada ya shuguli ya uzinduzi kukamilika, walioketi kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi AMREF Editha Temu, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Mkuranga, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Serengeti Richard Wells na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima. Waliosimama kutoka kulia ni Ofisa wa Mambo ya Ndani SBL, Imani Lwinga, Mkurugenzi wa Mahusiano SBL ,Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa Mahusiano EABL Brenda Mbathi,Mmoja kati wa waliokuwa katika msafara wa Mama Kikwete na Meneja Masoko SBL Tanzania , Nandi Mwiyombella.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Serengeti Richard Wells, kisoma risala fupi pamoja na kumakaribisha mgeni rasmi Mama Salma Kikwete.
Mama Salma Kikwete akipiga makofi pamoja na Mkurugenzi wa SBL, Richard Wells (Kulia) na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Adam Malima (Kushoto) mara baada ya kuzindua mradi wa mradi wa maji,Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani leo.
Hapa Mama Salma Kikwete akikata utepe.

MKE wa Rais Mama Salma Kikwete jana amezindua mradi wa maji katika Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani uliosimamiwa na Shirika la AMREF huku fedha za uichimbaji wa kisima hicho zikiwa zimetolewa na Kampuni ta East African Breweries Limited (EABL) Foundatin , Kiwanda cha Bia Serengeti (SBL).


Akizungumza mara baada ya kuzindua mama Kikwete alisema “Tukio la leo ni la muhimu sana kwetu sote hasa kwa wananchi wa Mkuranga, kwani maji ni nyenzo muhimu katika kumudu maisha ya jamii zetu.


Kuna usemi usemao ‘Maji ni Uhai’ ikimaanisha kuwa ukosefu wa maji huathiri sana maisha ya binadamu na nikikwazo kikubwa katika upatikanaji wa maendeleo” alisema Mama Kikwete.


Lakini katika nchi yetu tunafahamu waathirika wakubwa panapotokea ukosefu wa maji ni wanawake na wasichana ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.


Ninayofuraha kushudia wadau mbalimbali nchini wakiongeza wigo wa kuwekeza katika kuhakikisha jamii zetu zinapata huduma muhimu ikiwamo maji.


“Katika hotuba yenu mmeniarifu kwamba mradi huu umeweza kujenga visima virefu , vifupi , matanki ya kuvunia maji ya mvua pamoja na miundombinu ya usafi, vyote vitawanufaisha wananchi 270,000”.


Huu ni mfano mzuri ambao unafaa kuigwa na Mashirika mengine hivyo nawapongeza na kuwashukuru tena East African Breweries Limited (EABL),Foundation na Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa kuonyesha Njia.


Kuwepo kwangu hapa ni faraja kubwa sana kwani Taasisi yangu ya WAMA pia ina lengo la kuchangia katika maendeleo ya elimu, afya, na uchumi kwa wanawake, watoto pamoja na wanajamii walio katika mazingira magumu.


WAMA pia imetekeleza mradi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vikundi vya akina mama vya hapa Wilayani Mkuranga.


Tuliweza kutoa mafunzo ya uxzalishaji paprika nay a utunzaji mifugo kwa wanajamii 134 katika eneo hili. Taasisi yetu ya WAMA pia imekuwa ikisaidia ujenzi wa shule za sekondari , mabweni pamoja na upatikanaji wa umeme na maji katika sekondari.


Tunapenda kuwakaribisha wadau wote wanaopenda kushirikiana nasi katika kuleta maendeleo katika nchi yetu ili tushirikiane kwani naamini kuwa duniani kuna rasilimali za kutosha kuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayeshindwa kwenda shule kwa kukosa fedha, hakuna mwanamke anayepoteza maisha yake wakati wa kujifungua, hakuna mtoto anayezaliwa akiwa na maambukizi ya UKIMWI.


Mwisho alimalizia kwa kusema “Nawaomba wananchi wa Mkuranga mtumie msaada huu mlioupata vizuri.Tunzeni hivyo visima vya maji ili viweze kuwasaidia,Pia nawaomba muongeze juhudi katika kujiletea maendeleo , ongezeni ubunifu katika kutumia rasilimali mlizozipata ili kufikia maendeleo endelevu.


Na baada ya kusemsa hayo machache napenda kutamka kuwa mradi huu wa Water of Life umefunguliwa.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti Richard Wells alisema kuwa anajisikia fahari kubwa kwa Kampuni yake kutoa fedha na kuchangia huduma ya kijamii kama walivyofanya Mkuranga.


Alisema licha ya kuwa lengo la mradi huo lililenga kusaidia hospitali ya Wilaya ya Mkuranga pia nyumba zaidi ya 72 wameweza kuvuta maji.


Wakatihuohuo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini pia Mbunge wa jimbo Mkuranga Adam Malima ambaye alikuwepo katika hafla hiyo ameishukuru Kampuni ya Serengeti kwa kuwawezesha wakaazi wa Mkuranga na kuwapelekea huduma muhimu ya maji.


Pia aliongeza kwa kuwaaambia wakazi wa Mkuranga wawapeleke watoto wao shule ili wapate elimu itakayowasaidia katika mambo mbalimbali.


Aliongeza kwa kusema kuwa pia anawakaribisha wadau na wafadhili kujitokeza katika kuchangia Taasisi ye WAMA ambayo imejikita katika mambo manne makuu nayo ni elimu, afya, kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.


Baada ya kusindua hapa wakishangilia kwa kupiga makofi Mama Salma Kikwete katikati kilia ni Mkurugenzi wa SBL na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Adan Malima.
Wakielekea eneo ambapo Mama Salma Kikwete alikata utepe.




Hapa Mgeni Rasmi alikuwa akisubiriwa kwa hamu leo asubuhi.

No comments:

 
 
Blogger Templates