serengeti breweries yazindua kinywaji chake cha Tusker Malt Lager usiku wa kuamkia leo jijini dar.

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua bia yake ya Tusker Malt Lager,Mgeni wa heshima katika uzinduzi wa kinywaji Tusker Malt Lager,pichani kati Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko,Dr Cyril Chami akicheeerzzzzz na baadhi ya viongozi wa kuu wa kampuni ya SBL,Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells,Katibu Mkuu wa viwanda,biashara na Masoko Bi.Joyce Mapunjo,na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bi.Caroline Ndungu pamoja na Mkurugenzi wa Mahusiano SBL,Teddy Mapunda,hafla hiyo fupi imefanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya hoteli ya Kempinski,jijini Dar.
Meza kuu ikicheeerrrzzzz na wageni waalikwa usiku huu,mara baada ya kinywaji hicho murua kabisa chenye kimea 100% kwa wateja wanaopenda ubora wa aina hiyo,kuzinduliwa usiku wa kuamkia leo ndani ya hoteli ya Kempinski na kuhudhuria na watu mbalimbali.
Mgeni wa heshima katika uzinduzi wa kinywaji cha Tusker Malt Lager,Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko,Dr Cyril Chami amefafanua mambo kadhaa ikiweo na kuipongeza hatua ya kampuni hiyo ya SBL ya kuzindua kichwaji cha Tusker Malt Lager,amesema kuwa kuzinduliwa kwa bia hiyo ni ishara nzuri kwa Taifa,kwani itaongeza ushindani na kutoa fursa kwa watumiaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells amesema kuwa wanafurahi kuzindua kinywaji hicho ambacho kinajulikana kwa uhalisia na ubora wake,chenye kimea 100% kwa wateja wanaopenda ubora wa aina hiyo,ameongeza kuwa Tusker Malt Lager ni bia bora yenye medali ya dhahabu ya Monde Selection Gold Medals na ni bidhaa halisi ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikifurahiwa na wateja wa Uganda,Rwanda,Burundi,Kenya na sasa Tanzania.Amesema kuwa hii inaonyesha kuwa hii ni bia halisi ya Kiafrika na ina sifa zote za ubora.Bwa,Wells amebainisha kuwa SBL itaendelea kuwajali wateja wake katika mipango ya biashara zake na pia itaendelea kuwekeza zaidi ili kukidhi mahitaji ya Wateja.
Mkurugenzi wa Masoko SBL,Bi.Caroline Ndugu akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa usiku huu ndani ya hoteli ya Kempisk,amesema kuwa uzinduzi wa bia ya Tusker Malt Lager haa nchini Tanzania ni dhahiri kuwa SBL iko makini na soko la Tanzania na itatumia nafasi iliyopo kuwekeza zaidi na zaidi kwenye soko ili kujiimarisha kibiashara.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Baranaba akizikongo nyoyo za wageni waalikwa usiku huu,wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Tusker Malt Lager.
Wasanii wa THT wakiiongozwa na Lina (kulia) wakiimba kwa pamoja.
Mc wa shughuli hiyo,Taji Liundi akitoa muongozo kidogo kwa wageni waalikwa.
Walimbwende wakikatiza jukwaani wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Tusker Malt Lager usiku wa kuamkia leo.
Burudani ya asili pia ilikuwepo kuwatumbuiza wageni waalikwa.
Wageni waalikwa wakishangaa kiaina supraiiiiiiizzzziiiiii ukumbini kabla ya kinywaji cha Tusker Malt kuzinduliwa usiku wa kuamkia leo ndani ya hotel ya Kempinsk jijini Dar.
Kikundi cha ngoma ya asili katika picha pamoja kabla ya kuanza kutumbuiza.
Wageni waalikwa mbalimbali wakipata vinywaji taratiibu kabla ya uzinduzi rasmi kufanyika.
wageni walikwa wakibadilishana mawazo huku wakipa vinywaji taatiiibu.
Mkurugenzi wa Mahusiano SBL,Teddy Mapunda akitoa maelekezo kwa Mc wa shughuli hiyo,Taji Liundi kabla ya shughuli nzima ya uzinduzi haijaanza.
Mgeni wa Heshima Pichani wa pili kushoto ni ,Dr Cyril Chami akizungumza na wakurugenzi waandamizi wa SBL,kabla ya uzinduzi wa kinywaji cha Tusker Malt Lager kufanyika,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells,Mkurugenzi wa Mahusino,Teddy Mapunda na kulia kabisa ni MKurugenzi wa Masoko SBL,Caroline Ndungu.
Wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali walikuwepo pia kushuhudia uzinduzi wa kinywaji cha Tusker Malt Lager usiku wa kuamkia leo ndani ya hoteli ya Kempinski,jijini Dar.
Ama kwa hakika ukumbini palipendeza na kuvutia zaidi kama uonavyo pichani.
Wageni waalikwa wakijiandikisha kwa ajili ya kuingia kushuhudia kinywaji cha Tusker Malt Lager kikizinduliwa usiku wa kuamkia leo.

Post a Comment

0 Comments