DR. SHEIN NDIE URAIS MTEULE ZANZIBAR


MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM, DK. ALI MOHAMED SHEIN (PICHANI) AMESHINDA URAIS WA ZANZIBAR KWA MUJIBU WA MATOKEO YA TUME YA UCHAGUZI ILIYOTANGAZWA SASA HIVI ,AMBAPO DR. SHEIN AMEWEZA KUIBUKA MSHINDI KWA ASILIMIA 66.4%


MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AKUBALI MATOKEO NA KUIPONGEZA CCM NA MGOMBEA WAKE. ANAHUTUBIA HIVI SASA NA KUMKUBALI DK. ALI MOHAMED SHEIN KWA KUPATA RIDHAA YA WAZANZIBARI KUWAONGOZA KWA MIAKA 5 IJAYO.


HATA HIVYO MAALIM SEIF AMESEMA KUNA DOSARI ZINAZOTOKANA NA BADHI YA MAOFISA NA KUMUOMBA RAIS MTEULE KUWA MWANGALIFU NA HILO ILI NCHI ISIFIKE PABAYA.


AMESEMA KATIKA UCHAGUZI HUU HAKUNA MSHINDI AMA MSHINDWA. MSHINDI NI MZANZIBARI. NA KAMUOMBA RAIS MTEULE AHAKIKISHE HILO ILI HALI YA HEWA ISIJE KUCHAFUKA.


ANAMALIZA HOTUBA NA KWENDA KUMPA MKONO DK. SHEIN HUKU VIFIJO NA NDEREMO VIKIUMUKA KATIKA KILE KILICHOITWA MATUMAINI MAPYA KWA ZANZIBAR.


DK. SHEIN ANAITWA KUONGEA SASA.ANAINUKA NA KUELEKEA KWENYE KIPAZA SAUTI.


UKUMBI UMEJAA MSISIMKO SI WA KAWAIDA. ANAMFAGILIA MAALIM SEIF KWA HOTUBA FUPI LAKINI NZITO, ANAAHIDI KUSIMAMIA VYEMA UUNDAJI NA UENDESHAJI WA SERIKALI YA MSETO NA KUKUBALIANA NA MAALIM SEIF KUWA HAKUNA MSHINDI ILA WAZANZIBARI WOTE KWA MUSTAKABALI WA MAENDELEO YA VISIWANI.

Post a Comment

0 Comments