Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE
wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia (TLP) ameshinda kesi ya kupinga matokeo
ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo
kupitia chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Lyatonga Mrema .
Mbatia
ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa mlalamikaji (Mrema) kuamua
kufuta shauri hilo kwa hati maalumu iliyowasilishwa katika mahakama kuu
ya Tanzania Kanda ya Moshi huku akikiri kumtambua Mbatia kama mbunge
halali wa jimbo hilo.
Mbali
na utambuzi huo Mrema pia amekanusha maelezo pamoja na ushahidi wake
aliowasilisha mahakamani hapo dhidi ya Mbatia,wananchi wa jimbo la Vunjo
pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini ambazo zilitajwa
mahakamani hapo wakati wa ushahidi wake.
Ukiwasilisha
hoja mahakamani hapo mbele ya Jaji wa mahakama kuu Lugano Mwandambo ,
upande wa mlalamikaji ukiongozwa na wakili January Mkobogho ulieleza
kuwa pande mbili katika shauri hilo wamefikia makubaliano nje ya
mahakama.
Wakili
Mkobogho aliiomba mahakama kuona makubaliano hayo ambayo yako katika
maandishi kama alama kwa mujibu wa makubalinao waliyoafikiana baada ya
kuingizwa na kupokelewa mahakamani hapo kama madai.
Alisema
kwa kuwa kesi hiyo ya uchaguzi ikiwa na maslahi mapana ya umma na kwa
kuwa mlalamikiwa wa pili na watatu waliunganishwa kwenye shauri hili kwa
mujibu wa sheria aliomba kila upande ubebe gharama zao.
Wakili
Mkobogho alieleza kuwa kutokana na pande zilizokuwa zinakwaruzana
wameamua kukaa na kumalizana wenyewe na kwamba haoni sababu za
mlalamikiwa wa pili na watatu kutokubeba gharama zao wenyewe.
Jopo
la mawakili sita wa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili , Mohamed
Tibanyendera uliileza mahakama hiyo kwamba wanaungana na mtoa maombi kwa
maslahi ya umma na kwamba wanakubali kila upande kubeba gharama zake.
Wakili
mkuu wa serikali Mark Muluambo akisaidiana na wakili wa serikali
Grayson Orcado , alisema wamesikia pande zote na wameafiki kuhusiana na
uamuzi huo kutokana na kesi hiyo kuwa na maslahi kwa umma.
Alisema
upande wao hauna pingamizi na maamuzi hayo na kwamba wamekili kupokea
nakala na wataisoma na kuipitia vizuri, na kutokana na mlalamikiwa wa
pili na watatu walitumia gharama katika kesi hiyo waliiomba
mahakama walipwe nusu ya gharama hizo.
Baada
ya kusikiliza maelezo ya pande hizo mbili Jaji Mwandambo alieleza
kupata maelezo kuwa mlalamikaji amekiri kwamba kesi hiyo hainafaida
yeyote kwa wana Vunjo na kwamba amekubali kuwa tuhuma zake zote
alizokuwa nazo juu Mbatia na watu wote aliokuwa anawahusisha na kesi
hiyo kuwa amezitengua .
Jaji
Mwandambo alieleza kuwa mlalamikaji pamoja na yote aliyoyasema pia
amekiri kuwa mbunge wa sasa wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia alichaguliwa
kwa kura halali na alipata kura nyingi dhidi yake.
Nje
ya mahakama Wakili Tibanyendera alisema haikuwa kazi rahisi kufikia
maridhiano haya na kwamba ushawishi mkubwa umefanyika baada ya Wakili
anyemtetea Mrema kumueleza ukweli mwenendo wa shauri hilo.
“Tumefanya
kazi ya kuwashawishi wateja wetu ,Mrema amekiri katika maandishi
yaliyosajiliwa leo mahakamani baada ya kuona kwamba kesi hii haina faida
kwa wana vunjo,amekiri na kutengua tuhuma zake zote alizotoa dhidi ya
Mbatia,wafuasi wake na taasisi nyingine.”alisema Tibanyendera.
“Hoja
kubwa ilikuwa ni kupinga matokeo ya Ubunge,Mrema kwa maandishi amekiri
kwamba Mbatia alichaguliwa kihalali na akapata kura nyingi kihalali,hayo
yamo katika amri wa mahakama,”alisema Tibanyendera.
Akizungumza
mara baada ya kufikiwa kwa uamuzi huo Mbunge wa jimbo la Vunjo,James
Mbatia alisema Chama chake kina aamini katika itikadi za utu na kwamba
amemsamehe na hata dai gharama za kesi hiyo.
“Tungeweza
kumdai Mrema gharama kubwa,tangu kuletwa kwa kesi hiyo mahakamani,mimi
sitamdai Mrema hata senti moja,nimemsamehe Mrema kwa sababu ni mpiga
kura wa jimbo la Vunjo,nisingependa kuona anadidimia zaidi lazima ni
mlee vizuri mzee wngu Mrema,”alisema Mbatia.
“Gharama
za mawakili talipia asilimia 50 za mawakili wa upande wetu,Mrema
amekubali kulipa sehemu ndogo ya malipo ya mawakili wetu, tungeendelea
tungeweza kuuza hata nyumba zake, sasa atalipa Milioni 40 na tayari kwa
hatua ya kwanza mawakili watapewa Mil 15 ambazo tayari ziko
mahakamani,mwezi ujao atalipa Mil 15 na kabla ya mwezzi wa sita atalipa
Mil 10 “aliongeza Mbatia.
Mbatia
aliyekuwa amengozana na mawakili wake pamoja na baadhi ya wafuasi wa
chama cha NCCR-Mageuzi alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa
jimbo la Vunjo waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo .
“Niwashukuru
wananchi wa jimbo la Vunjo kwa ushirikiano na muda mwingi uliopotea
kwa ajili ya kufuatilia kesi hii ,yapo mengi ambayo tulitakiwa kuanza
kuyafanya lakini muda mwingi tulitumia katika kushughulikia shauri hili
“alisema Mbatia.
Upande
wa utetezi katika shauri hilo ulikuwa ukiongozwa na Mawakili Mohamed
Tibanyendra, Faith Sadala ,Youngsevior Msuya na Mike Kavala huku
Mawakili wa serikali wakiwa ni Mark Mluambo Helen Mwajage na Lilian
Machange.
Katika
uchaguzi huo Mbatia alitangazwa mshindi kwa kupata kura 60,187 huku
Mrema akiambulia kura 6,416, na mgombea wa CCM, Innocent Shirima, kura
16,097.
0 Comments