JK USO KWA USO NA KEPTENI KIONGOZI WA KIJESHI WA BURKINA FASO TRAORE JIJINI OUAGADOUGOU LEO

Rais mstaafu wa awamu ya nne na mjumbe maalum wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha ujumbe maalum  kwa kiongozi wa  Burki Faso Kepteni Ibrahim Traore Jijini  Ouagadougou na kushuhudiwa na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa nchi zote mbili.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Burkinafaso Kepteni Ibrahim Traore walipokutana leo tarehe 18 Aprili 2025 Jijini Ougadougue.
Mhe. Kikwete amewasilisha  salamu za Rais Dkt. Samia  Suluhu Hassan  ambazo zimeelezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo  ikiwa na lengo la  kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.
Kiongozi wa Burkinafaso Kepteni Ibrahim Traore.

Post a Comment

0 Comments