JIJENGE NA TWIGA CEMENT YAENDELEA KUNUFAISHA WATANZANIA


Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya saruji ya Tanzania Portland Ltd, Jamal Yahya (wa pili kulia), akikabidhi cheti cha ushindi kwa mkazi wa Iringa Fadhil Mbembe aliyeibuka mshindi wa mifuko 200 ya saruji, katika droo ya pili ya shindano la ‘Jijenge na Twiga Cement’, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 08.2016.  Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Meneja wa Usambazaji wa kampuni hiyo, Tumaini Joseph na Mkuu wa Idara ya Promosheni, Martha Haule.

Mkazi wa Iringa Fadhil Mbembe (kulia) aliyeibuka mshindi wa mifuko 200 ya saruji na mkazi wa Njiro Faibe Ng’odi aliyeibuka na mifuko 400 wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla hiyo.


DAR ES SALAAM

MKAZI  wa  Gangilonga  Mkoani  Iringa  Maria Kalinga mwenye um ri wa miaka 35 leo ameibuka kuwa mshindi wa kwanza  katika droo ya  Jijenge na Twiga Cement huku akishinda zawadi ya mifuko 600 ya Cement.

Akizungumza mara baada ya kupigiwa simu  na kupata taarifa za kushinda  Maria alisema yeye ni fundi msaidizi  wa ujenzi  kuwa alikuwa akitetemeka kutokana na kushinda zawadi hiyo.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa mkazi wa Kunduchi  Cassian Mihoza ambaye ajinyakulia mifuko 400 ya Cement huku nafasi ya tatu ikienda kwa Kennedy Owili  mkazi wa Jijini Mwanza ambaye amepata mifuko 200 ya Cement.

Washindi hao wamepatikana katika droo iliyochezeshwa  katika Kiwanda hicho  cha Twiga Cement  kilichopo Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.

Wakati huohuo  pia ilichezeshwa droo ya  mshindi wa mashine  ya kisasa ya kufyatulia matofali ambapo Pascal Karani  (25) mkazi wa Jijini Arusha  mfanyakazi wa kwenye bustani ya maua  amenyakua zawadi hiyo.

Droo hii ni ya tatu kuchezeshwa  huku washindi wengine wakiwa wameshapatikana.


John Badi Media Consultant/Blogger Hans PR Box 11717, Dar es Salaam E-mail: badijohn30@gmail.com/badijohn30@yahoo.co.uk Mob: +255784587088/0712155221 Blog: Daily Mitikasi Blog Link: www.johnbadi.blogspot.com For all of Photography, PR, Events Management and promotions activities.

Post a Comment

0 Comments