Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai 30, 2016
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza
vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye
makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Sambamba na Makonda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo mchezo wa
kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom Ilala, Dar es Salaam.
Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke
kwa pande zote mbili za wavulana na wasichana.
Kadhalika, wakuu wa mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika nao
watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao ambayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa
upande wa wavulana pia Arusha, Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.
0 Comments