Mtaalam wa Jiografia
kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani
kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo ambayo wana uwezo nayo ili
yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika chuo Kikuu Ardhi na vyuo vingine leo jijini Dar es
salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa
sekondari katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za masomo
wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu ya Sekondari.
Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa
Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Jangwani namna ambavyo Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi
wanaosoma katika chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga
mbalimbali yanayoihusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini ikiwemo uhifadhi
wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.
Baadhi ya wanafunzi
wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia na
kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi
wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo jijini Dar es salaam.
0 Comments