BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippinesa mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
Kimweri mpaka sasa amepanda
uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa
ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
bondia huyo mtanzania anaefanya
shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya
mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana
na akishinda mchezo uho
itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa
wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na
mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii
ya feb 26
Kimweri alitoa shukrani za
kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka
sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni
Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli ,
Rajabu Mhamila 'Super D'
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
ambao amekuwa chachu katika
mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama
anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake
ndipo kilipozikiwa
|
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi kocha wa Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini |
Wizara ya Nishati, Equinor wakutana Afrika Kusini
-
Wizara ya Nishati Tanzania imekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya
Equinor Tanzania AS kujadili, pamoja na mambo mengine, maendeleo ya
utekelezaji wa...
1 hour ago
0 Comments