Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan(kulia) mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.a , wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam.(Picha na Geofrey Adroph waPamoja blog)
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akizungumza na wananchama na wananchi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la Kinondoni waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akihutubia umma uliohudhuria uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akiwasalimia pamoja na kutoa neno kwa wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa ufunguzi rasmi wa kampeni za mgembea Ubunge jimbo la Kinondoni .
Mgombea udiwani kata ya Mwananyamala Bw. Songoro Mnyonge(kushoto) akitambulishwa kwa wananchi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge(kulia)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akimtambulisha Mgombea udiwani wa kata ya Kijitonyama, Ndg. Kamugisha wakati wa ufunguzi wa kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni
Mgombea udiwani kata ya Tandale Bw Tamimu akitema vidonge kwa wapinzani.
Bw. Massawe ambaye ni mgombea udiwani kata ya Ndugumbi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo
Mgombea Udiwani kata ya Magomeni Ndugu Bujugo akiwaomba kura wananchi waliofika kwenye mkutano huo na pia kuwapigia wabunge pamoja na raisi kupitia chama cha CCM
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kushoto) akipokea kadi ya CUF toka kwa bibi ambaye alikuwa ni kada wa chama hicho alidai hajaona manufaa yeyote kuwepo katika chama hicho ambapo alijitoa rasmi na kurudi CCM.
Bibi akiwasalimia wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Mzee Dalali akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao mwenyewe alidai umati ulifikia watu laki 250.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiendelea kumwaga sera
Umati mkubwa ukishangilia wakati wa mkutano
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiaga mashabiki wake baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.
NA KHADIJA KALILI
MGOMBEA wa Jimbo la
Kinondoni Iddi Azzan anayegombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi amewaambia
wakazi wa Kinondoni kwamba watasahau adha za mafuriko kwa sababu zipo fedha
kutoka Benki ya Dunia ambazo zitafanya kazi ya kuchimba na kuupanua mto Ng’ombe
na mto Msimbazi.
Alikwenda mbali kwa
kusema kwamba pesa ya fidia ya nyumba ambazo zitavunjwa ili kupisha upanuaji wa
mito hiyo ziko hivyo wanasubiri utekelezaji .
Alisema kwamba
anajivunia kwa kuweza kuusafisha mto Ng’ombe ambao ndiyo umekuwa chanzo cha
kuleta mamfuriko kutokana na wakazi wa waliojenga pembeni ya mto huo kutupa
takataka hovyo.
Azzan alisema hayo
katika uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika jumapili kwenye uwanja wa CCM
mwinjuma Mwananyamala Jijini Dare es Salaam.
Aidha aliongeza kwa
kusema kuwa serikali imetenga kiasi cha fedha ambapo kila kata itapata sh.mil 100 ambazo zitatumika kwa ajili ya
mikopo nafuu zitakazosaidia kinamama , vijana ili waweze kujiajiri.
Aidha alisema
kwamba endapo wananchi watamchagua na kurudi tena madarakani atahakikisha
wafanyabiashara wa Kinondoni ambao ni mama lishe, baba lishe , bodaboda na
wamachinga wengine waweze kufanya biashara zao bila kubughudhiwa huku
wakiwekewa utaratibu maalum.
“Machinga wote
watawekewa utaratibu mzuri ambao utawasaidia
kufanya biashara zao vizuri” alisema Azzan.
Naye Mstahiki Meya
wa Kinondoni Yusuph Mwenda aliposimama kumuombea kura Azzan aliwasisitiza
wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo kumchagua Azzan kwa sababu
ni mchapakazi .
“Tumesafisha sana
mito ya Ng’ombe, Tandale ikiwa ni katika kupambana na mafuriko licha ya
changamoto kubwa ni utupaji wa taka hovyo unaofanywa na wakazi hivyo mpigieni
kura ili aweze kuleta maendeleo zaidi na kutengeneza mazingira mazuri ya mito
na maeneo mbalimbali ya Kinondoni” alisema Mwenda.
Wakatohuphuo Azzan
alisema kwamba yeye kama Mbunge kabla
muda wake haujamaliza aliweza kuketi na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni na
kuunda sheria ndogondogo ikiwemo ya tika ambayo itawahusu wakazi wa jimbo hilo
watatakiwa kulipa kiasi cha sh.50,000 kwajili ya Bima ya afya ambapo mtu
akilipia atatibiwa kwa muda wa mwaka mmoja.
Azzan amewaahidi
wakazi wa kinondoni kuboresha zaidi afya ikiwemo hospitali ya Mkoa wa
Mwananyama na hospitali zingine na wilaya kama Tandale na Sinza.
Pia aliahidi
kujenga wodi za watoto wsachanga na
“Hivyo ili mpango
huu uweze kutimia chagueni Iddi Azzan kwa maendeleo na afya zenu kwa ujumla”
alisema Azzan.
Azzan anawania kiti
hicho kwa tiketi ya CCM ambapo tayari aliweza kushikilia kwa miaka 10
iliyopita.
0 Comments