Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya
Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha Lami.
Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa
upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete, Mbunge wa
Viti maalum kutoka Chama cha Wananchi CUF, Mbunge wa Simanjiro
Cristopher Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi na
viongozi wengine wa Kitaifa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa
barabara ya Mayamaya –Mela - Bonga Km 188.15. Wengine wanaoshuhudia
tukio hilo ni Mwakilishi wa Serikali ya Japan kushoto, katikati ni
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero,
Mama Salama Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema
Nchimbi.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli watano kutoka kulia
akicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Bicha kabla ya uzinduzi
rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa
kiwango cha lami.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Pombe Magufuli, Mama Salama Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Rehema Nchimbi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi
Gerson Lwenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa
Tanzania Dkt. Tonia Kandiero.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na
Mzee maarufu wa Wilaya ya Kondoa Balozi mstaafu Mustapha Nyang’anyi
kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Kulia
ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
0 Comments