Mwanaafa Mwinzago akipozi katika studio za Global TV Online.
Staa
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwizago
kutoka Kanda ya Kusini Mkoa wa Mtwara akiwa ndani ya Studio za Kampuni
ya Global Publishers Ltd wakati alipokwenda kufanyiwa Mahojiano na
Wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikiendi.
Mara
baada ya Kutua katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ambao ni
Wachapishaji wa Magazeti Pendwa Hapa Nchini Mwanaafa alipata nafasi ya
Kuongelea Namna ya Yeye alivyoweza Kuibuka Mshindi katika Shindano hilo
Kubwa na La Kwanza Kufanyika Afrika Mashariki na Kati lijulikanalo kama
Tanzania Movie Talents (TMT) huku akielezea Jinsi alivyoweza kupokea
ushindi alioupata Mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Ambapo
Fainali ya Shindano hilo Kubwa ilipofanyika na Yeye Kuibuka Kinara wa
Shindano hilo kwa Mara ya Kwanza.
Shindano
La Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano la Kwanza na Kubwa
Kufanyika kwa mara ya Kwanza Afrika MAshariki na Kati huku likiwa
limejinyakulia Sifa na Umaarufu wa Hali ya Juu kutokana na Umahiri wa
Uendeshaji wa Shindnao hilo ambapo Watanzania Wengi wamefurahishwa na
Uendeshaji wake uliojikita katika Utendaji wa Haki ambapo Mshindi
alipatikana kihalali.
Tanzania
Movie Talents (TMT) imepelekea sasa kuwafanya baadhi ya Watanzania
ambao waliokuwa wanajua kuwa shindano hili halitatenda haki basi Kuanzia
sasa wamejionea kuwa TMT ipo kwaajili ya kutoa haki. TMT ni shindano
ambalo kiukweli Limefungua Njia Kwa Watanznaia Ambao wana vipaji lakini
hawajapata nafasi ya Kuonekana.
Tanzania
Movie Talents (TMT) limeendeshwa takribani Miezi Minne huku kukiwa na
Changamoto Nyingi ambazo timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd
ambayo ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano hili Kubwa kujitahidi
kutatua changamoto hizo ili kuhakikisha Shindano hilo linafanyika kwa
Ustadi wa hali ya Juu na Utofauti.
Mbali
na Zawadi hiyo kubwa aliyoshinda Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwizago
zawadi nyingine ambayo amepata Kutoka Kampuni ya Proin Promotions ni
Kuwa Kampuni ya Proin itamsomesha Mwanaafa Mwizago katika Level Zote
kwasababu kampuni inatambua Umuhimu wa Elimu Kwa Mtanzania.
Sasa
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limemalizika kwa Mshindi mmoja
wapo kutoka kanda ya Kusini Mkoa wa Mtwara Mwanaafa Mwizago kuibuka
Kidedea na Kujinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
huku washiriki wengi wote tisa waliofanikiwa kuingia hatua ya Fainali
wakisubiri kucheza filamu ya Pamoja ambapo filamu hiyo itauzwa na
Kusambazwa na Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu
Tanzania ya Proin Promotions Ltd.
1 Comments