BENKI YA AZANI WAONGEZA ZAO JIPYA LA HUDUMA YA AKAUNTI YA DHAMIRA


MKURUGENZI mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili akimpa mkono mteja wa kwanza wa huduma mpya ya Akaunti ya dhamira Naomi Mapunda akaunti hii itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwezi uzinduzi uliofanyika jana Dar es Salaam.
(Picha kwa hisani ya Michuzi Media Group).
Na Mwandishi Wetu


MKURUGENZI mtendaji wa Azania benki Charles Singili, amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kujiwekea akiba kwa manufaa ya badae.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema kuwa utaratibu wa kujiwekea akiba utapungua tatizo la umasikini kwa wananchi.

Aliongezea kuwa, endapo wananchi wakiwa wakipatiwa elimu kuhisu faida za kutunza fedha itasaidia kupunguza hali ya umasikini uliopo sasa.

"Kwa kutambua matatizo yanayoikabili nchi yetu, Azania bank imeamua kufungua kaunti ambayo itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote" alisema Singili.

Singili aliongezea kuwa, akaunti ya Dhamira, itamsaidia mwananchi yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwenzi.

Aliongezea kuwa, akaunti hiyo inatafunguliwa na mtu ambae ametimiza miaka 18 ina kuendelea na itamsaidia kuweka riba kadri awezavyo.

"Dhamira ya akaunti hii, itamsaidia mwananchi kutimiza malengo au ndoto zao, pia kipindi cha chini kuweka akiba ni miezi 12," alisema.




   

Post a Comment

0 Comments