Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa
pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari
la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa
Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw.
Clement Mshana
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo
la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa
Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia matangazo la
TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana
Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa
moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya
Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani)
alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi
vinavyorushwa na Startimes alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li
Yunchao akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya
kuwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC)
alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia
matangazo (OB Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa
Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa
Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt. Fenella Mukangara
akijadiliana na jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw.
Jack Zhou.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya
makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa
moja (OB Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la
Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari
la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China
jana jijini Dar es Salaam.
0 Comments