Shaffih Dauda ameenguliwa tena kugombea wa nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kanda 13 ya Dar es Salaam.
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imetangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa
Bodi ya Ligi (TPL Board) utakaofanyika baadaye mwezi huu.
Uchaguzi wa Bodi ya TPL utafanyika Oktoba 25 mwaka
huu wakati ule wa TFF utafanyika Oktoba 27 mwaka huu. Kampeni kwa ajili ya
uchaguzi wa TPL Board na ule wa TFF zimeanza leo (Oktoba 18 mwaka huu) zitamalizika siku moja kabla ya uchaguzi saa
10 kamili alasiri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni
amewataja wagombea kwa upande wa TPL Board kugombea uenyekiti ni Hamad Yahya
Juma (Mtibwa Sugar), Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Said Abeid (Azam).
Wanaowania ujumbe wa Bodi ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na
Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui).
Wagombea kwenye uchaguzi wa TFF ni Athuman Jumanne
Nyamlani na Jamal Emily Malinzi (Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar
Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni
Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha
Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza),
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali
(Kanda namba 4- Arusha na Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo
(Kanda namba 5- Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo
(Kanda namba 6- Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge,
John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na Mbeya).
James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge
(Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba
Ndulane na Zafarani Mzee Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein
Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na
Singida), Farid Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma
Majala) na Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda
namba 12- Kilimanjaro na Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred
Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es
Salaam).
Mbwezeleni amewataka wagombea kufanya kampeni bila
kukashfu wenzao, kwani Kanuni ya Uchaguzi za TFF toleo la 2013 inatoa fursa kwa
Kamati ya Uchaguzi kuwaondoa wagombea wa aina hiyo kwenye uchaguzi.
0 Comments