Mgeni
Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa akitoa hotuba yake
wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo
Oktoba 2 mpaka Oktoba 5,2013.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey
Mlimuka akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi
wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini
Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye
Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,unaofanyika leo
kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Lulu Mengele akifafanua jambo juu
ya Muonekano wa Logo Mpya ya Mfuko huo iliyozinduliwa Rasmi leo kwenye
Ukumbu wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi
akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa
kuitika kwao wito kwenye Mkutano huo.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda wake wake mbele ya
Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa
Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana
Peter William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika
Shule ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na
Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF
ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha
ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo
Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia
kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana
Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana
na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF
ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili
kupoteza maisha.
Ilikuwa
ni huzuni tu wakati vijana hao wakitoa ushuhuda wao wa namna
walivyoweza kusaidiwa kimasomo na Mfuko wa Pensheni wa PPF pindi
walipoondokewa na wazazi wao.
0 Comments