Mtangazaji
wa Jamii Production Mubelwa Bandio akiwa na Wawakilishi wa wahusika wa
mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland
na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta
Kaiza
Ikizungumzwa
na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio
lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa
Afrika. Na inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani
Na
matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa
muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka
kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili
sasa kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani,
lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara
Asia.
Kiswahili
ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na
hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya
waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha
darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.
Wawakilishi
wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV
(Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha
Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami
katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.
KARIBU UUNGANE NASI
0 Comments