BONDIA
Yohana Mathayo 'Tembo Mtoto' amefariki dunia jioni ya leo akiwa
mazoezini kwakwe maeneo ya kigogo mbrurahati Dar es salaa kifo hicho
kilimkuta kwa gafla wakati akifanya mazoezi ya kujiandaa na mpambano
wake wa ubingwa uliopangwa kufanyika hivi karibuni ata hivyo Tembo mtoto
ametutoka taarifa za msiba huo zilizotolewa na kocha wake Kwame Mkuruma
zinasema kuwa mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao manzese na
huwenda akasafilishwa kwenda kuzikiwa kwao mkoa wa Tanga mungu ametoa na
mungu ame twahaaa mbele yake nyuma yetu kazi ya mungu aina makosa
tulikupenda sana ila mungu amekupenda zaidi tutakukumbuka daima milele
Yohana Mathayo 'Tembo Mtoto'
Mwenye rekodi ya kucheza
michezo 7 ya ngumi za kulipwa akiwa ameshinda mara 4 na kupigwa mara
moja na droo mara mbili Yohana alijiunga na ngumi za kulipwa mwaka 2011
ambapo mchezo wake wa kwanza kacheza na Seba Temba wa morogoro ambapo
alitoa nae droo na mchezo wake wa mwisho kucheza ni tareha 9,8,2013 akimpiga kwa T,K,O ya raundi ya pili bondia Shujaa Keakea
Mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Friends Corner Hall, manzese Dar es salaam
0 Comments