LONDON, England
“Diaz ni bingwa wa zamani wa Dunia na ni mpinzani hatari mno
ulingoni. Najua atakuja ulingoni akiwa na silaha kamili za maangamizi
nami nakuhakikishia niko tayari kwa lolote. Kasi yangu na ujuzi nilionao
ulingoni, nguvu zake na uzoefu alionao, vinalifanya hilo liwe moja ya
mapambano makali unayopaswa kuyashuhudia"
BONDIA Amir Khan amekiri kuisubiri kwa hamu Aprili 27, siku
ambayo atarejea ulingoni kumvaa Julio Diaz kwenye ukumbi wa Motorpoint Arena.
Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kwa Khan katika ardhi ya
Uingereza, tangu alipokubali kichapo kutoka kwa Paul McCloskey jijini Manchester
mwaka 2011.
Na Khan, 26 amethibitisha alivyoupania mpambano huo
kurejesha heshima yake iliyotoweka ulingoni – huku akisema: “Aprili 27 unaelekea
utakuwa usiku maalum.
“Imeshapita miaka miwili sasa tangu pambano langu la mwisho
katika ardhi ya nyumbani na sitasubiri kupanda tena ulingoni na kufanya vitu
adimu mbele ya mashabiki wangu.
“Diaz ni bingwa wa zamani wa Dunia na ni mpinzani hatari mno
ulingoni. Najua atakuja ulingoni akiwa na silaha kamili za maangamizi nami
nakuhakikishia niko tayari kwa lolote.
“Kasi yangu na ujuzi nilionao ulingoni, nguvu zake na uzoefu
alionao, vinalifanya hilo liwe moja ya mapambano makali unayopaswa kuyashuhudia.
“Yeye anaweza kuwa na amawazo kama waliyonayo wengine, nina
imani kuwa marejeo yangu katika ardhi ya Uingereza yatakuwa ya mafanikio
makubwa ulingoni.”
Diaz, 33, hajawahi kupigana kwa raundi 12 tangu alipopokwa
mkanda wa IBF – uzani wa ‘light’ alipoumana
na Juan Diaz mwaka 2007.
0 Comments