LONDON, England
“Nimezungumza mara
kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo
na Tyson yu tayari sasa kwa hilo.
Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia
Mei, Juni au Julai
BONDIA mahiri Tyson Fury amepania kupanda ulingoni kupimana
ubavu na Wladimir Klitschko kuwanuia ubingwa wa dunia kiangazi kijacho.
Fury, 24, bondia asiyepigika katika uzani wa ‘heavyweight,’ Jumamosi
hii anapanda ulingoni kumvaa Mmarekani Kevin Johnson jijini Belfast,
Ireland
ya Kaskazini.
Na promota wa pambano la Jumamosi Mick Hennessy amedai kuwa,
ushindi kwa Fury mwenye urefu wa futi 6.9, utampa fursa ya kuandaliwa pambano
dhidi ya Klitschko - bingwa wa mikanda ya WBA, IBF, na WBO.
Hennessy alisema: “Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir,
Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu
tayari sasa kwa hilo.
“Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika
kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai.
“Ujerumani ni nchi inayoweza kuwa kipaumbele chetu kupigwa
pambano hilo, lakini nimeshazungumza na wamiliki
wa Uwanja wa Old Trafford au Croke
Park,” alisema Hennessy.
0 Comments