MANAHODHA STARS WANG’ARA TUZO ZA VODACOM

Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja na msaidizi wake Aggrey Morris wameng’ara katika hafla ya kampuni ya Vodacom kukabidhi zawadi kwa wachezaji, klabu, waamuzi na makocha waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012.

Katika hafla hiyo iliyofanyika jana usiku (Juni 30 mwaka huu) hoteli ya Double Tree Hilton, Dar es Salaam, Morris anayechezea Azam aliibuka mchezaji bora wa ligi hiyo wakKila mmoja alizawadiwa sh. 3,312,500 katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye. Kaseja aliwashinda makipa Mwadili Ally (Azam) na Deogratias Munishi (Mtibwa Sugar) wakati Morris aliwashinda Haruna Niyonzima (Yanga) na Haruna Moshi (Simba).

John Bocco wa Azam aliyefunga mabao 19 ndiye mfungaji bora, refa bora ni Martin Saanya kutoka Morogoro ambaye aliwashinda Oden Mbaga (Dar es Salaam) na Amon Paul (Mara) wakati kocha bora ni Stewart Hall wa Azam aliyewashinda Charles Kilinda (JKT Ruvu) na Charles Mkwasa (Ruvu Shooting). Kila mshindi mepata sh. 3,875,000.
Timu yenye nidhamu bora ni Azam iliyopata sh. 7,750,000, mshindi wa tatu Yanga sh. 15,500,000, makamu bingwa Azam sh. 22,000,000 na bingwa Simba sh. 50,000,000.

Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewazawadia sh. 1,000,000 kila mmoja kwa wachezaji watatu vijana wenye umri chini ya miaka 20 waliofanya vizuri kwenye ligi hiyo.

Wachezaji hao ambao walikuwa kwenye vikosi vya kwanza vya timu zao ni Frank Domayo (JKT Ruvu), Rashid Mandawa (Coastal Union) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).
MARA YAKIONA CHA MOTO COPA COCA-COLA
Timu ya Mara imeuanza vibaya mwezi Julai baada ya leo asubuhi kupata kipigo cha mabao 5-0 mbele ya Dodoma katika mechi ya michuano ya Copa Coca-Cola iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Dodoma ambayo hiyo ni mechi yake ya nne mfululizo kushinda katika kundi hilo la C ilipata mabao yake kupitia kwa Vicent Tarimo aliyefunga dakika ya kwanza, Japhet Lunyungu (dakika ya sita), Ayoub Khalfan (dakika ya 65 na 89) na Abdul Madwanga (dakika ya 67).
Kundi A limeshuhudia Ruvuma ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Kusini Pemba katika mchezo uliofanyika leo asubuhi (Julai Mosi mwaka huu) kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Sunday Leonard (dakika ya nne) na Shanely Michael (dakika ya 44). Abdulatif Salim aliifungia Kusini Pemba dakika ya 90.
Nazo Iringa na Tanga zimetoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kundi B iliyochezwa Uwanja wa Tamco ulioko mkoani Pwani. Kagera imeitambia Tabora baada ya kuifunga mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam. Athuman Kassim na Shabani Ramadhan ndiyo walioifungia Kagera dakika ya sita na 88.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Post a Comment

0 Comments