JAMHURI YAWASILISHA USHAHIDI UMRI WA 'LULU'

Pichani ni msanii Elizabeth Michael 'Lulu' akishuka katika gari  la Askari Magereza.
Na Hellen Mwango (CHANZO NIPASHE) 
MAWAKILI upande wa Serikali kesi ya mauaji ya  aliyekuwa msanii nyota Steven Kanumba (28),inayomkabili  msanii  wa filamu Elizabeth Michael  'Lulu'  wamewasilisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam vielelezo  vya kuthibitisha  kwamba mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 18.

Vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani  ni pamoja na CD iliyorekodi  mahojiano  kati ya Mtangazji, Maelezo ya kuomba hati ya kusafiria,  na leseni ya udereva.
Pia umewasilisha  Mahakamani  hapo maelezo ya Polisi pamoja na maombi ya hati kusafiria  ambapo mshtakiwa  ameeleza  kwamba ana umri zaidi ya  miaka 18.
Keshi hiyo itasikilizwa Juni 25 mwaka huu mbele ya jaji Dk.Fauz Twaib Mahakamani hapo.
Juni 18 Mawakili wa nutetezi Peter Kibatala , Fugency Massawe na Kennedy Fungamtama waliwasilisha  vielelezo kwa  njia ya maandishi  kupitia kiapo.Katika ushahidi uliowasilishwa na baba mzazi wa Elizabeth  Michael Kimeleta  ameapa kwamba binti yake  hadi anatuhumiwa  kufanya mauaji , umri wake ni miaka 17.
Kalugira mama Mzazi wa Lulu anadai kuwa alimzaa mtoto huyo miaka 17 iliyopita  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam.
Upande wa Jamhuri unaoongozwa na Wakili nwa Serikali  Shadrack Kimaro .Lulu anakabiliwa na shtaka la  mauaji  dhidi ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu , katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments