Napenda kuwaarifu kwamba TPBC imetoa kibali cha mapambano sita (6) ya ubingwa wa taifa yatakayofanyika jijini Tanga tarehe 4/3/2012 siku ya jumapili katika ukumbi wa Community Center. Promota wa mapambano haya ni Ally Mwanzoa wa Mwanzoa Boxing Promotion ya jijini Tanga.
Washindi wa pamabano haya ya taifa watapambana na mabondia toka nchi za Kenya na Uganda kugombea ubingwa mpya wa “Jumuiya ya Madola wa Afrika ya Mashariki” unaotambuliwa na Bazara la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) ambapo Kamisheni za Ngumi za Tanzania (TPBC) Kenya (KPBC) na Uganda (UPBC).
Makao makuu ya CBC yapo jijini London, Uingereza la linajumuishwa na nchi zaidi ya 59 duniani zilizokuwa chini ya utawala wa Ufalme wa Uingereza.
Kamisheni hizi tatu za TPBC, KPBC na UPBC ni wanachama pekee wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) kutoka ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.
Ubingwa wa Taifa:
1. J.J. Ngotiko Vs. Ibrahim Habibu - Bantamweight (10 rounds)
2. Jumanne Mohammed Vs. na Juma Mokiwa - Featherweight.(10 rounds)
3. Haji Juma Vs. Omari Saidi - Flyweight weight (10 rounds)
4. Athumani Boxer Vs. Lucas Michael - Lightweight ( 10 rounds)
5. Saidi Mundi Vs. Saimon Zablon - Super Featherweight ( 10 rounds)
6. Zeberi Kitandula Vs. Bakari Shendeka - Super bantam ( 10 rounds)
Mapambano ya utangulizi yasiyo ya ubingwa.
1. Alibaba Ramadhani Vs. Juma Kihio Light Middleweight (8 rounds)
2. Hassan Ngonyani Vs. Puguto Omari Super Flyweight 6 rounds)
3. Patric Kimweri Vs. Issa Omari (light flyweight 6 rounds)
Imeandaliwa na;
Onesmo A.M.Ngowi
0 Comments