NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA KATIKA TAMASHA LA KURUKA KAMBA KUFANYIKA 9 DESEMBA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Kijiji Cha Makumbusho Emmanuel Ngala, anayefuata ni Mratibu wa tamasha hilo  Dennis Makoi,  Director  One World  One Rope Michael Fry na  Jump  Rope  Master Peter  Nester.
Na Mwandishi wetu 
KATIKA kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, Uongozi wa kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam umeandaa mashindano ya mchezo wa kuruka kamba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Emmanuel Ngala alisema kwamba mashindano hayo yameratibiwa na Denis Makoyi na yatashirikisha nchi za Afrika Mashariki.
Ngala ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mchezo wa Chama Cha Tenisi, alisema michuano hiyo ya kuruka kamba itawashirikisha washiriki 60 wa ukanda wa Afrika Mashariki na 10 wa kigeni, huku mmoja akiwa ni kutoka nchini Canada na 9 kutoka nchini Marekani.
Mashindano hayo ya aina yake yamepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kwa siku mbili, yaani kesho Ijuma, Desemba 9, na siku inayofuata, Jumamosi Desemba 10.

Wakati huohuo, muasisi wa mashindano hayo Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya One World One Rope, Michael Fry ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Naye Mkufunzi wa mchezo huo, Peter Nester ‘Jump Rope Master’ alisema kuwa, katika Tamasha hilo wataonesha mitindo na staili kemkemu ya kuruka kamba.
“Ni mchezo ambao unajenga mwili na afya kwa ujumla, ambako pia unachezeka katika rika na jinsia zote ila sisi tunautia nakshi zaidi na kuwa wenye mvuto kutokana na kuruka kwa kasi ya hali ya juu,” alisema Nester.
Katika tamasha hilo, kundi la wasanii kutoka Nyumba ya Vipaji (Tanzania House of Talent) ‘THT’, watakuwepo.

 Hapa wakionesha jinsi ya kuruka kamba  kama timu  moja.
Hapa wakiruka kamba kwa pamoja.
Hapa akiruka  kwamba huku akiwa amekaa chini.

Post a Comment

0 Comments