EWURA AIPA KIBALI KAMPUNI YA WIND EA CHA KUZALISHA UMEME WA UPEPO NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebo akimkabidhi leseni ya uzalishaji wa umeme wa upepoBw. Rashid Shamte ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Wind EA katika hafla fupi iliyofanyika jijini jana. kampuni hiyo imepewa leseni ya kuzalisha umeme wa upepo wa 100mw kwa kipindi cha miezi 30.
(Picha na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu.
MAMLAKA ya Nishati na Madini Nchini '' Ewura'' jana imeikabidhi Kampuni ya uwekezaji ya Wind East Africa Limited 'Wind EA', leseni ya kuzalisha umeme utakaozalishwa kwa upepo wa MW 100 ambao utaingizwa kwenye Grade ya Taifa.


Umeme huo huo utaanza kuzalishwa nchini punde mara baada ya jana kukabidhiwa leseni hiyo, uzalishaji utafanyika mkoani Singida huku Ewura ikitoa miezi 30 ya matazamino kabla ya kuipa kampuni hiyo leseni ya kudumu.

Akikabidhi Leseni hiyo kwenye ofisi za Ewura zilizopo Posta jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema kuwa kamapuni hiyo ni ya kwanza hapa nchini kuzalisha umeme wa Upepo.
Masebu alisema kuwa Serikali kupitia Ewura wametoa leseni hiyo ambayo itakuwa ya miezi 30 na baada ya muda huo kumalizika wataipa leseni ya kudumu kwa mujibu wa taratibu za nchini.

"Sheria inaruhusu wawekezaji binafsi hivyo kulingana na sheria tunatoa leseni kwa kampuni ya Wind EA ambayo ndiyo ya kwanza kuzalisha umeme unaotokana na upepo hapa nchini," alisema Masebu.

Alisema kuwa wametoa leseni hiyo baada ya kampuni hiyo kufuata taratibu zote ikiwamo ya mazingira ambapo wanacheti walichopewa na Baraza la Kudhibiti Mazingira 'NEMK'.

"Hii itakuwa ni moja kati ya Technologia zinazotumika hapa nchini kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme ambapo wataungana na Solar na Maporomoko ya maji katika uzalishaji huo, hivyo nafasi ziko wazi kwa wawekezaji wengine wenye vigezo," alisema Masebu.

Mkurugenzi Mradi wa Wind EA, Rashid Shamte alisema kuwa Tanzania itakuwa ni moja kati ya nchi zaidi tano za Afrika itakayonufaika na mradi huo ambao unagharimu Dola za Marekani 3.75 Bilioni.

Alisema kuwa mradi ni kwa ajili ya nchi zilizoendelea na ambazo zinaendelea ikiwamo Tanzania na kuongeza kuwa kwa hapa nchini ni kuzalisha umeme huo kwa muda wa miaka 30 ambapo wanashirikiana na Serikali ya Tanzania kwa msaada wa Benki ya Dunia.

Shamte aalisema kuwa eneo ambalo litatumika katika uzalishaji huo liko KM 10 kutoka Singida Mjini na kuzitaja baadhi ya nchi nchi ambazo Wind EA wamezalisha nishati hiyo kuwa ni Ghana, Nigeria, Gambia na Kenya.

Post a Comment

0 Comments